abdulahsaf
JF-Expert Member
- Aug 31, 2010
- 858
- 130
Wazanzibar tungekuwa mbali kama sio kujipakatisha kwa Muungano fake.Mimi nahisi hapa kuna mtego umetegwa na huenda kutokana na viongozi wetu wa Smz wakauingia na kutuingiza sisi kutokana na uzaifu wao wa kukumbatia Muungano usio na zamira njema kwa uchumi na maendeleo ya Zanzibar kama nchi yenye watu kidogo na ardhi ndogo.
Uhakika wa kupiga hatua ya maendeleo ya kujikwamua Zanzibar kiushumi na kimaendeleo tusahau? Hakuna sababu kwa nini Watanganyika wakatae Tanganyika yao au Serekali 3?.
Kama tungekuwa na mfumo wa Serekali 3 yani Serekali ya Tanganyika kwa mambo ya Tanganyika yasio ya Muungano na Serekali ya Zanzibar kushuhulikia mambo ya Zanzibar yasio ya Muungano basi ingepunguza utata na ulalamishi wa kero za Muungano?.
Lakini inaonekana wenzetu yote hayo hawayataki lengo ni kusema ni Serekali 2 kuelekea 1? Jee ikiwa hivi sasa Wzanzibar Watanganyika wanatuhukumu kutokana na udogo wa watu wetu na nchi yetu kusema haifiki hata mkoa moja wa Tanganyika, tukiingia ktk hio Serekali 1 status ya Zanzibar itakuwa vipi?. itakuwa ni Zanzibar kumezwa na kupoteza utaifa wake ndani ya Tumbo la Muungano wa Tanganyika ijitayo Tanzania kwa kulindwa na Sera za chama.
Tusahau Zanzibar kupiga hatuwa ya maendeleo kwa vile mambo yake yote yako undercontrol ya tanganyika na sirahisi Zanzibar kujikwamua kwa vile Serekali ya Tanganyika haipo na wenzetu ccm/smz huongozwa kwa itikadi ya sera za chama.
Kwani kuna ubaya gani kuwa na Serekali ya Tanganyika ikasimamia mambo ya Tanganyika tu? mbona Egepty inashiriki ktk jumuia ya AU na jumuia ya nchi za Kiarabu? kwa hio na Muungano wetu tunaweza kukutana kwa mambo yale tuliokubaliana kuungana.
Mimi nahisi lengo la Muungano wenzetu nikututawala kimpinu na Tayari viongozi wetu wameshakuwa mental slaves, kama hakuna Tanganyika lengo Wazanzibar nikuuza nchi yetu na kuwa utaifa wa Zanzibar kuwa nchi na Tanganyika kubaki na utaifa wao na power yao kwa jina la Tanzania.
Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibar wote