Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Leo hii, nimesoma habari kuwa Wafanyakazi wa TRL, wameamua kujichukukulia majukumu ya kuendesha na kuongoza TRL baada ya Rites kutoa notisi ya siku 60 kujitoa na Serikali kukaa kimya bila kutoa kauli inayoeleweka.
Ukimya wa Serikali ya Tanzania katika mambo ya msingi na kutatua kero za Wananchi unatisha!
Uongozi wa Serikali ya Tanzania inaelekea umelala usingizi wa Pono kama si kuamua kuwa haujali yule mpiga kura aliyeipa Serikali hii dhamana ya kuliongoza Taifa la Tanzania.
Anzia Ajira, Elimu, Afya, Usalama wa Wananchi, Maji Safi, Umeme, Msongamano wa Magari, kukosekana kwa Uwajibikaji, kuongezeka kwa Uhujumu na Ufisadi, ni kero kila kona na napenda kukataa na kuipinga kauli yangu ya wiki tatu zilizopita kuwa Tumeridhika na dhiki, tabu na mateso.
Ujasiri wa wafanyakazi wa TRL, hata kama tutadai eti haukuwa wa halali, naupongeza kwa kuwa tangu awali, Serikali yetu ambayo ni mbia mkubwa wa mkataba huu wa Shirika la Reli, imefumbia macho malalamiko ya Wananchi na hata mradi wenyewe wa Uwekezaji TRL haukufanyika kwa unyoofu pamoja na Serikali kuelezwa.
Wakati unaanza wadia ambapo Wananchi wanaamua kujichukulia hatua mkononi. Wanaamua kufanya kazi na kuchukua dhamana ya kuongoza na kuendesha nchi yetu kutokana na kukosa uaminifu na uvumilivu kutoka kwenye kauli hasi za Viongozi na Serikali.
Inasikitisha, inatisha na inadhalilisha, lakini itakapobidi, sitashangaa kusikia siku moja asubuhi kuwa Wananchi wamejitwalia Ikulu na Bunge na kuamua kujiongoza kwa matakwa yao wenyewe kutokana na kuchoshwa na Viongozi wazembe na Serikali isiyojituma wala kuthamini dhamana iliyopewa kuongoza Taifa la Tanzania!
Sichochei machafuko au watu kuvunja sheria, lakini ikiwa leo haki ya Mtanzania inawekwa majaribu kutokana na kiburi, uvivu na dharau kutoka kwa wale walioaminiwa kuongoza na kulipeleka Taifa letu katika njia iliyo sahihi, Mchungaji hatashangaa, wala kuwasikitikia wale watakaoondolewa madarakani kutokana na uzembe wao!