Habari za Jumapili watu wa Mungu.
Ni matumaini yangu mu wazima kabisa. Pole kwa yeyote mweye matatizo, ndio ubinaadamu. Niende kwenye mada.
Miaka kadhaa iliyopita tulipata kusikia kuhusu upatu unaitwa D9 Clubè na wengine tulifuatwa tuwekeze huko. Matomaso wengi kama mimi tukaogopa na kuacha kila kitu kiendelee tu kwa wanaotaka. Tukasema time will tell, ngoja tuone.
Sasa nimekuja hapa kutaka kujua, hii biashara ya upatu imeishia wapi? Siisikii ikitajwa tajwa sana siku hizi. Ndio kusema watu "wanapiga hela tu" au ukiona manyoya ujue keshaliwa?
Wakuu hebu tupeane ujuzi nini kimetokea.