Iko wapi ile CZECH REPUBLIC YA Pavel Nevded???

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Nlikua mmoja wa mashabiki wa timu ya Taifa ya Czech Republic kipindi cha nyuma kidogo enzi izo ikiundwa na Wakali kama Pavel Nevded uyu mtu alikua fundi sana anzia timu ya Taifa mpaka Juventus.

Wakali wengine kama Milan Baros mashabiki wa Liverpool wanamjua huyu mtu alikua mkali wao wa kutupia.

Na jamaa wao mmoja wakuitwa Jan Koller mrefu hivi na nguvu za kutosha kwa magoli ya vichwa alikua hatari sana,kama sikosei kakipiga pale Monaco/France na wakali wengine

Tangu icho kizazi kipotee Timu yao ya Taifa imekua haina mvuto sana kama ule wa zamani zaidi ya mkongwe Peter Szech na yule beki wao mwenye asili ya Ethiopia,nimekua siwafwatilia sana siku hizi.

Nini kimesababisha Jamhuri ya Szech kupotea kidogo kwenye soka japo kwenye michuano mikubwa kama World/Euro cup bado wanaonekana???
 
Eeeh bhana eeh
EURO 2004
peter Cech
Jan koller
Milan Baros

Hahaha, nakumbuka Czech ilipigwa goli na Ugiriki nikenda kulala hapo hapo, hawa jamaa walikuwa shda
 
Eeeh bhana eeh
EURO 2004
peter Cech
Jan koller
Milan Baros

Hahaha, nakumbuka Czech ilipigwa goli na Ugiriki nikenda kulala hapo hapo, hawa jamaa walikuwa shda
Timu ilikua imekamilika kila idara asee dimba la kati yuko Pavel Nedved mpaka raha.

Ugiriki akaja na style yake anakuchapa kamoja tu halafu hakirudi mpaka fainali anamchapa mwenyeji/ureno kamoja halafu anabeba ndoo

Viwanja kama Dragao, burudani sana

Ureno ya akina Deco/Figo/Rui costa
 
Eeeh
Bwana ile czech kama hawakuchukua kombe lolote miaka ile watasubiri.
Hahah
Ule mpira wa wagiriki ulikuwa wana kuvizia ila wakikupata tuu goli moja limetosha
 
Wanapotea taratibu wameshiñdwa kutoa vipaji vipya
Nawakumbuka sana Patrick Berger na Karel poborscky
 
Kila nchi lazima inakuwa na golden generation, ikiisha hiyo mpaka ije nyingine ni muda mrefu sanaaa. Nedved nilikuwa napendaga mikwaju yake
 
Eeeh
Bwana ile czech kama hawakuchukua kombe lolote miaka ile watasubiri.
Hahah
Ule mpira wa wagiriki ulikuwa wana kuvizia ila wakikupata tuu goli moja limetosha
Miran Baros anaibuka mfungaji bora na kubeba Golden boots,

Wagiriki walikua watata halafu hawakupewa nafasi kubeba kombe,anamfunga szech republic extra time

Magoli yao mengi vichwa na majina yao marefu
 
Kila nchi lazima inakuwa na golden generation, ikiisha hiyo mpaka ije nyingine ni muda mrefu sanaaa. Nedved nilikuwa napendaga mikwaju yake
Kabisa Ndugu kama Senegal ya Tony silva /Diof/Fadiga/Camara/Diop chini ya kocha marehemu kwa sasa Bruno Metsu,baada ya kizaz kile kuisha walipita kipindi kigumu sana naona sasa ndo wanarudi

Pavel Nedvedv alikua amekamilika
 
Umemsahau Henry Kamara mkuu, kumbuka ile Nigeria ya kina okocha, kanu, babangida, babayaro, njoo Cameroon ya etoo, mboma, song, hata Brazil, France, Portugal, kooote it's all about golden generation
 
Nlikua mmoja wa mashabiki wa timu ya Taifa ya Czech Republic kipindi cha nyuma kidogo enzi izo ikiundwa na Wakali kama Pavel Nevded uyu mtu alikua fundi sana anzia timu ya Taifa mpaka Juventus.
Jan Koller alikuwa anakipiga Borussia Dortmund. Historia yake alianza kama kipa na baadaye ktk timu ya Sparta Praha akabadilishwa kuwa striker. Aliweka historia amoja ktk mechi ya bundesliga kati ya Dortmund na Bayern msimu wa 2002-03 kuwa kipa aliyeokoa zaidi michomo baada ya kipa wa Dortumund Jens Lehmann kupewa kadi nyekundu na Koller kuamua kuingia golini. Alipata kuwa kipa bora wa wiki hiyo.
Binafsi ni moja ya mastriker niliotokea kuwaelewa sana.
 
Sikupata kuelewa hiyo story ya Jan koller kumbe ni Multi talented
 
Sikupata kuelewa hiyo story ya Jan koller kumbe ni Multi talented
Alianza kama keeper lakini wakamwona anaweza kuwa forwad mzuri ndio maana kwenye mechi yao na bayern alikuwa mkombozi alipoingia golini.
 
Eeeh
Bwana ile czech kama hawakuchukua kombe lolote miaka ile watasubiri.
Hahah
Ule mpira wa wagiriki ulikuwa wana kuvizia ila wakikupata tuu goli moja limetosha

Mfumo kama wanaotumia Atletico,wakikufunga goli haulirudishi.
 
Godin,Gabi,philipe Luis,Diego Simeone katengeneza ukuta mgumu sana ila juzi kati Sevilla kamfunga kamoja
Ndio hivyo hamna namna maana muosha naye huoshwa.
 
Aisee umenikumbusha mbali nadhani kugawanyika nako kumechangia maana sasa hivi kuna Czech na Slovakia zilishajitenga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…