Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Jana wkati taarifa ya uteuzi ya wabunge watatu iliyotoka Ikulu,
kuna kitu kimenishangaza.
Hivi lugha iliyotumika hapo chini ni sahihi? au Ikulu hawajui kiswahili?
MWISHO
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma
17 Novemba, 2010
Hapo kwenye red ndipo ningeomba kuelimishwa.
Hapo mwandishi anakusudia kutueleza kuwa yeye ni raisi msaidizi au ni mwandishi wa raisi msaidizi (means yupo rais msaidizi) kama alikusudia kutueleza yeye ni mwandishi msaidizi wa raisi alipaswa kuandika hivyo alivyoandika??
Kiswahili fasaha ni janga la taifa. Kuanzia ikulu, ofisi za serikali hadi vyama vya upinzani.
Ilani ya uchaguzi ya Chadema ilikuwa na makosa ya Kiswahili yaliyokithiri.
Sikuisoma ya Cuf lakini naamini hali ilikuwa vivyo. Ya Ccm ndo hayo tunayaona
Gaijin hayo sio makosa ya CCM ni makosa ya Serikali........au kuna kitu sikifahamu unataka kuniambia?
Ccm ndo ilotuwekea wazembe serikalini bila ya kujali uwajibikaji. Uzembe wa aina hii kwa nchi za wenzetu hamna kwa sababu Chama kinachoongoza serikali hakiwezi kuruhu watu wafanye makosa ya kizembe aina hii.
Tena Ikulu!