Ikulu ilizuia Vigogo 3 Kufikishwa Mahakamani


Hizo habari chanzo chake siwezi kukitaja hapa ingawa ungependa nitaje lakini iko siku habari hii itatoka live kwenye vyombo vingine vya habari. Si unajua Mafisadi ndo madai yao hayo (Remember Mwanahalisi kuambiwa watoe chanzo cha habari ili wapate sababu ya kuwasulubu watu? Hata madai ya EPA Spika si alitishia kumpeleka Polisi Dk. Slaa ili awakilishe huo ushahidi kwenye ofisi yake? LAkini mwisho wa siku ilikuwaje, si ilibainika kuwa ni kweli hata bila Dk Slaa kupeleka ushahidi Bungeni na badala yake akaendeleza libeneke Mwembeyanga Tandika?
 

Ibrah,
Sidhani kuwa kuna anayetaka chanzo chako cha habari ila sidhani kama kutaja majina ya waliofikishwa mahakamani (hao mawaziri), kuwa nayo ni siri. Hii habari yako ina mapungufu mengi sana, ni nafuu ukaulizie tena huko ulikoipata kama hukutunga au uachane nayo maana inakuharibia sifa yako kuwa mzushi.

PCCB au polisi hawawezi kumchukulia hatua waziri au PS yeyote, wa sasa au wa zamani, bila kuwasiliana na bosi wao, JK, kwanza hata kama yuko Iceland.
 

Mkuu Ibrah, binafsi nimekusoma sana. Hivi hii habari si mpya na iliandikwa katika magazeti ikiwamo RaiaMwema na nimeweka link katika post yangu hapo juu page ya kwanza. na watu waliichangia hapa JF... Binafsi nina uhakika mkubwa na hiyo habari hadi wahusika na kila tukio. Kuhusu kwenda mahakamani, si kesi zote watu wanaonekana na kwa hili si kwamba waliotinga mahakamani ni watuhumiwa bali wanasheria wa DPP office na PCCB na baada ya mawasiliano ndipo Luhanjo akaingilia. Habari ndio hiyo, kwa kuwasaidia someni post za mwanzo
 



Dpp Kuridhia Mashtaka Dhidi Ya Vigogo Kesi Za Pccb?

Raia Mwema - Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi

Mramba na Yona kushitakiwa!! | Jambo Blog Network
 
Mbona hii habari siyo ngeni jamani... tumejua kwa miezi sasa kuhusu ugumu wa Ikulu kuridhia hawa jamaa kushitakiwa. Majina yalishawekwa hata hapa hakuna cha siri tena. Halisi amewawekea link sidhani kama watu wanajaribu kuangalia... hakuna jipya, hatuhitaji maneno tena, tunachohitaji kuona ni jamaa wamesimama kizimbani! Hayo mengine ni irrelevant.
 
Yaani mwizi anaomba asikamatwe hadi muda wake wa kustaafu utakapofika?

Wote wezi!!! Hivi we hujapita Kariakoo au pale Jangwani, kibaka akikuibia simu anakimbizwa na vibaka wenzake na wewe ukiwafuata wanakwenda kukumalizia walivyobakisha. Luhanjo ana yake kwa hiyo sikushangaa kusikia hayo. Nimesema nitaanza baadaye ya Luhanjo kwa wakati wake mwafaka.
 

Mheshimiwa Kubwajinga,

Ile interview ya Mbowe vipi? utafanya lini?
 
Mbona hii habari siyo ngeni jamani... tumejua kwa miezi sasa kuhusu ugumu wa Ikulu kuridhia hawa jamaa kushitakiwa.

Mkuu,

Unakumbuka uliwahi kukataa kwamba Rais hayuko juu ya hawa ma DPP, na Wanasheria Wakuu, na law enforcers wengine ? Sasa Ikulu kuridhia na kutoridhia mashitaka wamepata wapi nguvu hizo ?
 

 
"mabangusilo" wanaandaliwa kwa ajili ya sympathy vote 2010.

Ni kweli kabisa, lazima kuna mpango wa kutoa baadhi ya mafisadi kafara kwa ajili ya uchaguzi wa 2010
 
Ni kweli kabisa, lazima kuna mpango wa kutoa baadhi ya mafisadi kafara kwa ajili ya uchaguzi wa 2010

Patamu patakuwa pale ambapo mabangusilo watatolewa na bado watabwagwa kwa kishindo!

Kwani bilioni moja Tarime si wameiramba bado wakafanya kweli? kinachotakiwa hapa ni watu waelewe, pesa wakileta wailambe afterall ni hela yetu wenyewe waliyo tufisadi, baada ya hapo kwenye sanduku la kura wanafanya kweli, ikifuatiwa na ulinzi madhubuti ili kura zisiibiwe!
 

Hii habari inaonyesha wazi vita ya ndani kwa ndani...Ukiangalia kwenye red highlight utaona ni mzee Rukhsa wanamwambia anyamaze kwani na yeye wanaweza kumweka kwenye chain yao ya ufisadi..Na msisitizo wakaweka kwenye kauli mbiu yao kuwa nchi HAITATAWALIKA kama wakishughulikiwa....Na kurudia kuwa awamu ya pili this and that..Ya tatu wala haina noma na ya nne.

Watazunguruka sana lakini nadhani hawazisomi alama za nyakati..Kwamba hata ndani ya miaka kumi ijayo udhalimu waliokwisha ufanya ambao wananchi sasa wanaufahamu hauwezi kupita hivi hivi tu bila uwajibikaji.

Wakidhani porojo zitamaliza haya mambo..Then wanaishi kwenye dunia yao ya kufikirika.
 
 
Jamii Forum isiwe ni siri. Sasa Vigogo watatu maana yake nini. Inatakiwa isemwe wazi kuwa Mafisadi watatu Mgonja, Yona na Mramba.

Hii serilkali ni ya mambo madogo madogo tu ambayo ni none issues. yale maissues yenyewe haina usemi wowote..
 
Unaelewa nyani hucheka mkia wa mwenzake. Hata uzushi wa taarifa ni sehemu ya ufusadi.kila la kheri kwa uzushi.wengine twapenda habari za ukweli na zenye uhakika ndipo tuweze kuchangia mawazo yetu
 
Kubwajinga,
Lisemwalo li.. kama halipo, la..
Kila jambo uanza kama tetesi na kukutwa limekuwa jambo.
Moto uonekana kwa kuona moshi kwanza.
Tusubiri tuone!
 

Mkuu you are very right.they must stop playing us.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…