Mh. Lusinde amesema Ikulu sio wodi ya wagonjwa na kumnanga dk Slaa.
Awali ilielezwa ña mbunge mmoja kuwa zikianzishwa mbio kati ya Kinana,Maalim Seif na Slaa basi padri ataishia hospitalini kwa afya mgogoro. Spika nae akachagiza kuomba VIP marathon ili watu wasiofiti kiafya wajulikane.
Bora tuchague Rais Mzee ili muda wake ukiisha akalee wajukuu kuliko kumchagua Rais kijana na muda wake ukiisha atataka kujiongezea mda huku akijiona bado ni kijana.
Mbona wapo waliokuwa na kifafa na wakadumu katika nafasi zao bila shida na hakuna aliyewahi kuwanyanyapaa. Maneno ya mtu kama Lusinde ni bora kuyachunguza sana kabla ya kuyafanya nukuu kwani yanaweza kuwa na damage upande wake bila yeye kujua
Wogonjwa wengi wapo kijani jamani pale ikulu wapo na hata mawaziri wengi ni vimeo huyo lusinde sijawahi kusikia akichangia hoja ya kutetea wananchi siku zote huchangia ujinga tu na mipasho.
Hakuna alie ona kesho,wala mtu asikae akadhihaki afya ya mwenzie kwani yote hiyo iko mikononi kwa mwenyezi mungu.
Hao wenye pesa na madaraka wengi wao wanakula dawa kama si ya BP basi ya maradhi mengine,wanalala pazuri wanakula vizuri lakini furaha ya nafsi hawana,usingizi mie na wewe tutalala kwa amani lakini wao usingizi mpaka ameze DAWA....