Ikulu yachachamaa habari ya Jk kugeuzwa mradi

yeah.. maana wameandika kwa kireeeefu lakini wameshindwa kusema kama hafla hiyo ilifanikiwa au vipi.. halafu mbona sijasikia zinduka nyingine.. au ndio ukishazinduka unaruhusiwa kuzimia tena?

Simples challenge kama hizi, hawaziwezi wao wanabaki kulialia, unafikiri hayo mengine humo ikulu wanafanyaje?

Ikulu inakuwa kama kundi la Zee comedy. Huwezi kukuta any good and convicing explanations kutoka kwa hawa jamaa. Tunajiuliza nani kambadilisha mwenzake? Je ni Kikwete ndio anasababisha haya, je ni hawa washauri wake? au imetokea coincidental kuwa ikulu wote wakawa sawa kabisa.

I believe kulinda heshima ya ikulu yaliyotokea kwenye ule uzinduzi ulitakiwa uambatane na watu fulani kufukuzwa kazi.

Yakianza mambo ya mahakama hizi statement zitakuwa zinabadilika badilika, ili mradi ku-fool wananchi.

Ndio hawa akina January Makamba wanataka ubunge!
 
Mhshimiwa Rais Kikwete anaanza kupata taarifa na anajipanga vizuri, ila bado tunapigana mbaka huyu mpinga maendeleo ya vijana Ruge Mutahaba na mtandao wake waweze shughulikiwa , hata wakikanusha ila meseji teali imefika na kama walidhaji watu wajinga jibu limepatiokana na wamesha gundua kuna kosa nadhani kwa busara watajipanga vizuri.
 
yeah.. maana wameandika kwa kireeeefu lakini wameshindwa kusema kama hafla hiyo ilifanikiwa au vipi.. halafu mbona sijasikia zinduka nyingine.. au ndio ukishazinduka unaruhusiwa kuzimia tena?


Mkuu sii kwamba unaruhusiwa bali ni unalazimishwa kuzimia tena. Maana tusipozimia ili tuzinduliwe mradi utakuwa umejifia.
 

Well said MKJJ,nadhani wewe utakuwa mchezaji mzuri sana wa chess ama drafti lol!...Back to the point,majibu yao waliyoyatoa kuhusiana na tuhuma za mh rais kugeuzwa mradi ni sawa kabisa na maelezo ambayo yangeweza kutolewa na kampuni yeyote ile,kama siyo neno "ikulu",na wakati wakijaribu kumprotray kama rais wa "nchi",bado maelezo ni kama vile ikulu ni kampuni, ni kama maelezo tu kuwa kampuni haikuhusika na haya ama yale na wala rais wake asihusishwe na mikataba ambayo kampuni yao haihusiani nayo,na kwamba wawakilishi na wafanyakazi wa kampuni hiyo yani "Ikulu" hawana makosa yoyote yale ya kujinufaisha kinyume na matakwa halisi ya mkataba huo na kwamba mapato yote ya kampuni hiyo ni halali....Na kwamba yote yaliyofanywa na wafanyakazi hao wa kampuni yalikuwa na baraka za rais wake na yalikuwa chini ya taratibu za kampuni hiyo na mikataba inayohusiana na mapato ya kampuni hiyo...Sasa wakati wanaambiwa kuna watu waliitumia ofisi ya raisi maybe kwa manufaa binafsi,walitakiwa waone haueni ila watafute namna nyingine ya kujinasua lakini si hii michezo kama kombolela ya watoto na sasa kukimbilia nyuma ya public office na wakati vitendo ulivyofanya ni sawa tu na a private company ama a corporation...Sasa wanapobisha,then swali lako linakuwa muhimu,wapi proceedings ama mapato?

Tunajuwa kunamikataba,wao wanadai kuwa mikataba yao haiingiliani na mikataba ya kina sugu,lakini ukweli ni kwasababu wanataka kujinasua,lakini kuna uwezekano wa contractual business interference,kama kulikuwa na mkataba wa awali,lets say wa sugu na kampuni x,halafu kampuni "Ikulu" ikatumia influence flani na kuuvunja mkataba wa awali kati ya sugu na kampuni x,na huku kampuni "ikulu" ikijua wazi kuwa sugu na kampuni x are in contract,basi sugu ana kesi dhidi ya kampuni x,ama wafanyakazi wa kampuni "ikulu" ama he can sue both (lol)

Hii nchi wanaichezea sana hawa watu,watulie na wasikilize wasidhani watu ni wajinga,waweke ukweli wazi wasidanganye watu,dunia hii ya sasa ya JF bado wanatuletea viini macho.....Ikulu walitakiwa waseme sisi hatujamgeuza JK mradi na si kuelezea kisiasa eti habari hii si kweli whtasoever.....Wanasema tamasha liliandaliwa na wizara,je hayo ni kweli?

Sasa wenye kushutumiwa kwamba wamenufaika ndiyo wenyewe wamejibu lakini in the way kama walitaka ionekana si wao wameiandika,badala ya kusema watu wanaofanya kazi kwenye ofisi ya rais wangetakiwa waseme sisi tunaofanya kazi kwenye ofisi ya rais hatujanufaika na mapato hayo kwasababu hii ama hile....Once again they think we're fools coz bado wanatumia ofisi ya rais kujibu tuhuma kuhusiana na matumizi yao mabaya ya ofisi ya rais badala ya wao kutoa majibu ya kuridhisha kwamba ni kwavipi hawaitumii ofisi ya rais vibaya kama inavyoonekana wazi.
 

Mangi Mangi Mangi....brevity is the soul of wit my friend.....
 

Nani anayetengeneza terms of reference katika ushiriki wa Rais/Ikulu? huyo ndo wa kwanza kupewa lawama.
 
Nilishawahi kutanabaisha hapo awali kwamba, mchezo alioucheza JK wa kuteua wasaidizi wasanii na wasio waadilfu hapo IKULU utamgharimu sana, haya ni mwerndelezo tu wa mengi ambayo yamekwishasemwa na kutabiriwa na wana JF.
 
Hapa Ikulu inasema hivi

Mheshimiwa Rais alishiriki kama mgeni rasmi tu katika shughuli hiyo. Siyo yeye Mheshimiwa Rais ama Ikulu ilishiriki katika maandalizi ya uzinduzi huo kwa namna yoyote ile.

Halafu Ikulu inajisahau tena inasema hivi


Halafu kitu kinakwenda kwenye Vyomboi yva Habari na Hukuna Mwandishi yeyote anayehoji Mkanganyiko huu
 

Nakubaliana na mkuu mmoja aliyesema mapaka tufike oct tutayasikia na kuyaona mengi. Hivi ikulu ipi hiyo inayotoa taarifa inaliyojaa utata na inayotuacha na maswali mengi bila majibu. Nashawishika kuamini kuwa "ikulu" imetumika kama rubber stamp kwenye taarifa hiyo.

Mimi na upeo wangu huu mdogo sipati picha halisi ya hizo data za malaria kama inauwa watu zaidi ya 291 kwa mwaka na kwa kila lisaa limoja wanakufa watu 10, pls waungwana nisaidieni hapo.

Noamba pia kufahamu "ikulu ya wananchi" ni ipi. Wanasema pia kuwa muheshimiwa alifika pale kama mgeni rasmi lakini maofisa wa ikulu walioshiriki kwenye maandalizi waliagizwa na Muheshimiwa Raisi.......(which is which)

Naogopa kufikiria kuwa mpaka ifike oct Muheshimiwa wetu asijekuvikwa "koti zuri la hariri" ambalo wananchi wake hawalioni, maana wamejaa dhambi.
 
Nani anayetengeneza terms of reference katika ushiriki wa Rais/Ikulu? huyo ndo wa kwanza kupewa lawama.

I hope siyo yule yule aliyesimamia mambo ya ambulance, hoteli arusha, mtumbwi songea, helikopta.. I hope its not the same.
 
Sasa wanaeleza kitu gani ambacho ni kipya?

1. Mradi ulikuwa wa akina MR 11
2.Clouds wakaingilia kati - Ruge
3. Tamasha likafanyika sijui usiku ?
4 Watu wakalipa kiingilio na fedha ikishia kwa hao waliochangisha.
5.Ukawa ni mradi uliokamilika ukiongozwa na Presida.

Wajasiriamali wajanja kweli kweli. Nyie ikulu mnalala tu na kuanza kupinga pinga vitu vilivyo dhahiri. Mradi huu ulifanikiwa kwa sababu Presida alikuwepo.
 
Kama yupo mtu anayo maslahi yake katika mpango huu na uzinduzi wake basi asimhusishe Rais wa Jamhuri ya Tanzania au Ofisi ya Rais, Ikulu.


Si wanasema kulikuwa na viingilio mbona hamuweki bayana vile viingilio nani alipewa tender ya kukusanya na zilitumika vipi zile pesa na kwa ajili ya nn? Kama pesa zilichangishwa hamuoni kama Rais kageuzwa mradi wa watu wachache?
 

Ebwaneeee Bongo tambalale kweli vp mkuu na sisi tuanzishe tamasha la ukimwi tumwite rais si tutatengeneza mkwanja.? Sasa baada ya hilo tamasha la maralia nini kilichofuata hapo si akina Ruge wameweka chao mfukoni na wanyonge wanaendelea kufa na maralia nasikitika jamaa angu juzi mtoto wake kafariki Mwananyamala kwa ajili ya maralia.
 
Rais kaagiza......???????????........!!!!walifanya hivyo kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais ya kufanikisha shughuli hiyo!!!!

Kwa nini asihusishwe kama kuna harufu isiyoeleweka ndani yake???
......................laaaaaaaaaaana hii itaisha kweli??.......................................
 
Hivi hiyo hafla ilifanikiwa kiasi gani?

Na hili ndilo jambo la maana zaidi la kujiuliza. Nimekuwa nikitafakari sana hili, tangu pale tulipoambiwa tuwe kizazi cha mwisho kukubali kufa kwa Malaria...kauli ambayo ina utata kweli! Kisha likaja tamasha...hivi walitaka at the end of the event wawe wamefanikiwa kufanya nini? Kugawa vyandarua? Kuhamasisha ununuaji wa vyandarua? Kuhamasisha kuharibu mazalia ya mbu? Kuhamasisha watu kutumia dawa mseto? AU?

Na je? Waliandaa au kupanga viashiria (indicators)vya mafanikio? Lile tamasha lilisaidia nini? Vijana ambao nafikiri walikuwa walengwa walipotoka pale walihamasika? Kufanya nini? Hivi walihamasika? Kuna wakati naona the positive idea behind hii kampeni lakini nahisi pia ina utata mkubwa katika utekelezaji na hivyo mafanikio ya lengo halisi yana mashaka makubwa kuchangia katika kupambana na malaria
 

Nimekugongea thax cause ndivyo ilivyokuwa na aliuza ikulu ni mtoto wa balozi ndo hapo J to the K kampa ruge ambaye chini ya kapeti ni entertainaa wake esp. totoz😕
 

shhhhhhhhhhhhhh angalie wasije kukupoka hiyo 'idea' yako, mkuu fide. On the same token, inabidi uanze na kutengeneza kiungio hapo kitalu namba moja
 

The two paragraphs seems contradictory.

Was it necessary for Ikulu to do what is in the next paragraph?
 
Ikulu wana tatizoo kubwaa katika utendajii wao.. Hii taarifa tuu ina mapungufuu lukuki!!

Hivi tatizoo ni watendaji wa ikulu (kiuwezoo kufikiri na kungamua mambo) au kuna walakini fulanii!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…