Ikulu yatangaza kupokea majina ya wajumbe wa Bunge la Katiba

Ikulu yatangaza kupokea majina ya wajumbe wa Bunge la Katiba

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,501
Hii ni taarifa ya Ikulu ya hivi Punde

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Taasisi mbali mbali za kijamii, vyama vya kitaaluma na vyama vya siasa vipatavyo 50 hadi leo, Jumanne, Desemba 31, 2013, vimewasilisha majina ya watu wao ambao vinapendekezwa wafikiriwe katika kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Taarifa iliyotolewa leo mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa taasisi hizo zimewasilisha majina yao kwa mujibu wa mwaliko uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa makundi yaliyobainishwa katika Kifungu cha 22(1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Sura ya 83).

Taarifa hiyo imesema kuwa makundi hayo 50 yaliyowasilisha majina yanayopendekezwa kwa ajili ya uteuzi yanatokana na barua 169 zilizopokelewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar.

Makundi ambayo yamewasilisha majina ni yafuatayo: Shirika la Wasaidizi wa Jamii Kabila la Wagogo, Tanzania Association of Social Workers (TASOWA), Teachers and Student Forum Tanzania, Tanzania Women Teachers Association, Umoja wa Wanawake Wajane Wilaya ya Karagwe na Kyerwa (UWK), Tanzania Peace and Development Society, Better World Organization (BWO), Youth Focus and Development, Association of Traditional Medicine Man, Registered Centre for Good Governance and Development in Tanzania, Chama Cha Kijamii (CCK), CHANETA na Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania.

Makundi mengine ni Legal Aid Iringa Village, Tanzania Kilolo Orphans and Social Development Organization, Legal aid and Social Welfare Association, Legal and Human Right Centre, Tanzania Lift Initiative NGO, Kilolo Paralegal Unit, Women Development and Social Activities Association, Defence of Human Right/Citizen Rights, DAWSEN Trust Fund, Baruti Development Association (BADEA), Living Hope Ministries Trust, EFATHA Ministry, Bethel Assemblies of God Tanzania, Muslim and Christian Brotherhood Society, Baraza Kuu la Waislamu wa Kondoa – Tanzania na Jesus Temple Inner Transformation News.

Taasisi nyingine ni Jumuiya ya Waithna Asharriyyah Tanzania, Rehmatfi Sabilillah Trust of Tanzania, Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), National Reconstruction Alliance (NRA), Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Demokrasia Makini, African Progressive Part – APPT Maendeleo, National League for Democracy, Tanzania Film Federation, Taasisi ya Maendeleo ya Utamaduni, Al-Amoud General Enterprises, Blue Belt and Water Sources Control, Community Development Training Institute – Tengeru, Tanzania Medical Student Association, Tanzania Sea Farmers Union, Medical Association of Tanzania, Chama cha Wastaafu wa Mbinga, Union of Tanzania Press Clubs, Umoja wa Wanawake Tanzania, Alliance for Tanzania Farmers Party, Tanzania Social Economic and Environment and Wellbeing.

Kwa vile mwisho wa kupokea orodha ya majina hayo ni tarehe 02 Januari, 2014, Balozi Sefue ametoa mwito kwa makundi mengine ambayo hayajawasilisha orodha hiyo kufanya hivyo kabla muda uliowekwa kuisha. Aidha, wakati wa kuwasilisha ni muhimu kuzingatia vigezo vilivyowekwa na sheria na kama vilivyofafanuliwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 443 lililochapishwa tarehe 13 Desemba, 2013. Vilevile ni muhimu kuzingatia kuwa majina yanayopendekezwa na Taasisi au makundi yaliyoainishwa kwenye sheria na siyo mtu binafsi kujipendekeza mwenyewe.

Kwa wale watakaojipendekeza wenyewe wajue kuwa watakuwa wanakwenda kinyuma na maelekezo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Desemba, 2013
 
LIST NZIMA NASHANGAA SIONI CHAMA CHA WAFANYAKAZI (TUCTA)

Nilitegemea sana sana wafanyakazi na wakulima kuona maoni yao,muda mrefu wapo kimya sana sana,na wawekezaji wanakuja kuanzisha makampuni hapa na kujilipa mishahara minono huku wazawa wakilia kuwa eti sheria ya Nchi hairuhusu mzawa kulipwa fedha nyingi hii ndo inatokea Viwandani na Migodini.
 
LIST NZIMA NASHANGAA SIONI CHAMA CHA WAFANYAKAZI (TUCTA)
Nilitegemea sana sana wafanyakazi na wakulima kuona maoni yao,muda mrefu wapo kimya sana sana,na wawekezaji wanakuja kuanzisha makampuni hapa na kujilipa mishahara minono huku wazawa wakilia kuwa eti sheria ya Nchi hairuhusu mzawa kulipwa fedha nyingi hii ndo inatokea Viwandani na Migodini.
Bado wengi sana mkuu lakini bado wana saa 48 kabla ya deadline kufika.
 
Hii ni taarifa ya Ikulu ya hivi Punde

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Taasisi mbali mbali za kijamii, vyama vya kitaaluma na vyama vya siasa vipatavyo 50 hadi leo, Jumanne, Desemba 31, 2013, vimewasilisha majina ya watu wao ambao vinapendekezwa wafiriwe katika kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.


Wewe ni Mwana Mpotevu tena sana si kidogo.
 
Wapo waliopanga kuhujumu mchakato wanajiita kadima aka chadema.
 
Upande wa Znz majina wanawakilisha wapi? sijawaona. Ilamutikio mpaka sasa inatisha.
 
Naona ccm, cuf na chadema bado hawajapendekeza majina ya wajumbe wa bunge maalumu la katiba! Ni vizuri wawasilishe haraka majina hayo.
 
Wewe ni Mwana Mpotevu tena sana si kidogo.
Dah we Mama unasoma neno kwa neo....Tuombe Mungu mchakato huu ukamilike salama maana tunaingia kwenye kipindi kigumu cha bunge la Katiba. Wahusika watangulize zaidi maslahi ya Taifa kama alivyosema Mh Rais wetu.
 
Back
Top Bottom