Ikulu yatoa agizo...nguvu ya pesa itumike kuhakikisha Katiba ya Chenge/Sitta inapita,

Ikulu yatoa agizo...nguvu ya pesa itumike kuhakikisha Katiba ya Chenge/Sitta inapita,

Ni hatari siyo kidogo....na inaonyesha ni kiasi gani brains za serikali tukufu ya CCM zinavyochemsha bongo 🙈
 
Mbombo ngafu,

kwa mtindo huo basi katiba ya Sitta itapitishwa kwa mtutu wa bunduki.

Tuombe kheir

Barubaru, kwa maoni yangu ni kuwa katiba itapita. Kwa bara huku sifuri, hakuna upinzani wa maana, pona ya sauti ya watu iko Zanzibar, Zanzibar wananchi wanaweza kuikataa, huku bara umeona usanii unaoweza kufanyika na unafanyika.
 
Salva Rweyamamu bila aibu, haya au soni anasema hakuna tatizo kwa proposal anayoidai.

Hapa tuna tatizo kubwa sana nchini.
Kwamba Ikulu inaona kununua na kuhonga watu ni jambo la kawaida. Ikulu haijaona tatizo la rushwa hata kidogo, halafu Ikulu hiyo hiyo inakemea rushwa.

Salava anasema, kuna bajeti ya upande wa Yes kwa mujibu wake. Sijui bajeti ya upande wa no itatoka wapi. Salva haelewi kuwa katiba imesusiwa na wala si suala la yes au no, ni kwamba ni haramu tu.

Halafu Ikulu ina mabilioni ya pesa za kampeni za hongo, Ikulu haina pesa za vitanda muhimbili.

Kuna tatizo kubwa sana nchi hii, na bila wananchi kusimama tutasikia siku moja fungu la bajeti likienda kuhudumia send off ya mtoto wa Salva. Ikulu itasema hakuna tatizo! hawaoni matatizo kabisa.
Ikulu ya Tanzania!!!
 
kama tuliaminishwa kuwa ukombozi wa mtanzania utategemea jembe na shoka,
kwasasa ukombozi wa maskini huyu utategemea PANGA, SIME, MKUKI, MSHALE, RUNGU na silaha nyingine yeyote ya jadi kupambana na wanyama waharibifu wa mazao yao shambani.
 
Back
Top Bottom