Salva Rweyamamu bila aibu, haya au soni anasema hakuna tatizo kwa proposal anayoidai.
Hapa tuna tatizo kubwa sana nchini.
Kwamba Ikulu inaona kununua na kuhonga watu ni jambo la kawaida. Ikulu haijaona tatizo la rushwa hata kidogo, halafu Ikulu hiyo hiyo inakemea rushwa.
Salava anasema, kuna bajeti ya upande wa Yes kwa mujibu wake. Sijui bajeti ya upande wa no itatoka wapi. Salva haelewi kuwa katiba imesusiwa na wala si suala la yes au no, ni kwamba ni haramu tu.
Halafu Ikulu ina mabilioni ya pesa za kampeni za hongo, Ikulu haina pesa za vitanda muhimbili.
Kuna tatizo kubwa sana nchi hii, na bila wananchi kusimama tutasikia siku moja fungu la bajeti likienda kuhudumia send off ya mtoto wa Salva. Ikulu itasema hakuna tatizo! hawaoni matatizo kabisa.
Ikulu ya Tanzania!!!