Ikungi na ujenzi wa vyumba vipya 29 vya madarasa

Ikungi na ujenzi wa vyumba vipya 29 vya madarasa

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry C. Muro leo tarehe 14/12/2022 amefanya ziara ya ukaguzi na kupokea taarifa ya ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa 29 katika shule 16 za majimbo ya Singida Mashariki na Singida Magharibi ujenzi ambao umegharimu shilingi milioni 580.

Muro akiwa pamoja na Mhandisi wa Halmashauri Millinga na Afisa Elimu Sekondari Mwalimu Ngwano wametembelea shule zote 16 na kujiridhisha na kazi inayoendelea ya ujenzi ambapo mpaka kufikia leo ujenzi umeshakamilika kwa asilimia 99.

Katika ziara hiyo Muro pia amejionea zoezi la uwekaji wa viti na meza katika kila darasa, kazi ambayo inaendelea kwa madarasa yote 29 na kusisitiza zoezi lazima liwe limekamilika mpaka kesho asubuhi tayari kwa ajili ya makabidhiano kwa Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba siku ya Alhamisi tarehe 15/12/2022.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,
Ikungi.
14/12/2022

IMG-20221215-WA0000.jpg
IMG-20221215-WA0001.jpg
IMG-20221214-WA0002.jpg
IMG-20221214-WA0003.jpg
IMG-20221214-WA0008.jpg
IMG-20221214-WA0007.jpg
IMG-20221214-WA0006.jpg
IMG-20221214-WA0005.jpg
IMG-20221214-WA0004.jpg
IMG-20221214-WA0011.jpg
IMG-20221214-WA0010.jpg
IMG-20221214-WA0009.jpg
IMG-20221214-WA0013.jpg
 
Back
Top Bottom