Ila ninyi Masai wana vituko jamani

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Juzi kati nikiwa kwa fundi msafisha viatu pale Kibaha Maili moja nikiwa sina hili wala lile ghafla nilishuhudia kituko cha karne hahahahaha!

Ipo hivi mama wa kimasai wale wanaouza dawa za miti shamba ilionekana akitaka kumuita kwa jina lake jamaa mmoja aliyekuwa na wajihi wa ki Ustaadh.

Sasa basi katika mahangaiko ya kutaka kuita jina la yule Ustaadh ilionekana dhahili alilisahau na ndipo yule akaona isiwe tabu na ghafla akaanza kupayuka "WEWE MUSIGITI πŸ˜‚" akimaanisha wewe msikiti yaani wewe Ustaadh!
 
[emoji23][emoji16][emoji16][emoji16][emoji2][emoji2]
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Dogo utarogwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…