Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Ilani ya chama cha siasa
Ni mwongozo na mkataba kati ya chama cha siasa na wapiga kura Kwamba chama cha kisiasa kinamwahidi mpiga kura mambo kitakachomfanyia kama kikipata ridhaa yake kupitia sanduku la kura kwa kipindi fulani.
- Kwamba huna nini na nitakupatia nini
- Kwamba umekosa nini na nitakupa nini
- Kwamba umepungukiwa nini na nitakuongezea nini katika kipindi chote cha ridhaa ya uongozi wa chama husika
Hitaji kubwa la mwananchi kwenye ilani husika ni kama:
- Elimu bora kwa wote
- Maji safi na salama kwa wote
- Miundombinu inayoweza kutumika nyakati zote
- Nishati bora na nafuu kwa wote
- Lishe bora kwa wote
- Afya na matibabu bora na nafuu kwa wote
- Uhuru na haki kwa wote
- Maendeleo ya watu na vitu nknk
Hivyo basi chama cha siasa kinapokuja kuomba ridhaa ya uongozi ni lazima kije na ILANI inayogusa hayo maeneo. Na kikishapata ridhaa ni LAZIMA kitekekeze ilani husika kwa vitendo katika muda wake wote wa ridhaa. Muda wa ridhaa ukishatimia inabidi chama kirudi kutoa mrejesho wa mkataba wake wa ilani na wapiga kura:
- Chama kiliahidi nini na kimefanya nini
- Chama kilifaulu wapi na kimefeli wapi na kwasababu zipi
- Si jambo la afya kama chama kikitoa ahadi mpya wakati kuna ahadi za nyuma hakijaziteKeleza Walau kwa asilimia 50
Slogan za vyama
Hizi ni kichocheo cha ilani husika! Ni kauli mbiu..hizi ndio huhamasisha matokeo vitendo ya ilani katika vyama vya siasa
Kwa mfanoa hapo nyuma kwa chama cha CCM kilikuwa na slogan ya ARI MPYA NGUVU MPYA NA KASI MPYA, hii ilikuja wakati wa JK wananchi wakiwa wamekatishwa tamaa na uongozi uliopita wa BM. Na baada ya hapo ikaja ARI ZAIDI..NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI.
Baada ya kutoka hapo tukaja na SLOGAN ya HAPA KAZI TU.
Kuna shida kubwa kwenye hizi kauli mbiu...Je zinatungwa na chama ama na mgombea? Je zinaakisi kilichomo kwenye ilani ama ni mapenzi binafsi ya mgombea? Hapa kazi tu ni slogan tata..kuanzia kwa wafanyakazi, wakulima mpaka wafanyabiashara!
Tukiwa kwenye awamu nyingine ya kuomba ridhaa ya wananchi
Je, ilani ya chama tawala ni ipi?
Je, slogan mpya ni ipi?
Kuelewa ni jambo la kwanza na kutekeleza ni jambo lingine!
ILANI NA KAULI MBIU NI LILA NA FILA...lakini mpaka ujue maana yake