Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Ilani ya CCM yadanganya
Ilami ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2010 imesheheni takwimu zinazoikinzana, imegundulika.
Katika ilani hiyo, ambayo anatumia mgombea Jakaya Mrisho Kikwete kuomba ridhaa ya kuendelea na urais, inaelezwa kuwa uchumi umekua kutoka asilimia 4.5 mwaka 2005 hadi asilimia 6.7 mwaka huu.
Lakini takwimu za serikali na washirika wake Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) zinaonyesha kuwa kiwango cha asilimia 6.7 kilifikiwa mwaka 2005 na siyo mwaka huu.
Hata kiwango cha asilimia 4.5 ambacho inadaiwa ndicho utawala wa kikwete ulianza nacho mwaka 2005, hakipo, kwani tayari wakati huo, serikali iliyokuwa inamaliza ngwe yake ilikuwa tayari imefikia asilimia 6.7.
Kwa hiyo, ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka huu ilipaswa kuonyesha utendaji wa serikali kufaulu au kushindwa kuanzia asilimia 6.7 kwenda juu au kurudi chini. Haifanyi hivyo.
Ripoti ya WB ya mwaka 2007 kuhusu biashara na uchumi nchini ilisema, ..uchumi wa Tanzania ulikuwqa ukikua kwa wastani wa asilimia tano hadi sita katika kipindi cha kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.
Basil Mramba, aliyekuwa waziri wa Fedha katika serikali ya Mkapa, aliuambia mkutano wa mwisho wa Bunge la bajeti (2005) mjini Dodoma, kwamba uchumi wa Taifa umekua kwa asilimia 6.7.
Alisema, mheshimiwa Spika, utawala wa Awamu ya Tatu umepata mafanikio makubwa ya kiuchumi. Kwa mfano, uchumi umekua kutoka asilimia 4.2 mwaka 1996 hadi asilimia 6.7 mwaka 2005.
Kwa mantiki hii, miaka mitano ya utawala wa Kikwete imekuwa ya makitaimu; bado uchumi uko palepale alipouacha rais mstaafu Benjamin Mkapa. Hii ina maana Kikwete ameshindwa kuinua uchumi wan chi ..
Habri zaidi katika Mwanahalisi la leo.