Pre GE2025 Ilani ya chama cha siasa itakayokosa haya ipigwe chini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

proisra

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2012
Posts
215
Reaction score
158
UTANGULIZI: Mwaka huu 2025, Tanzania itafanya Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge wake. Ni muda muafaka kwa vyama vya siasa kujinadi na sera zitakazoleta Maendeleo kwa Taifa letu ndani ya miaka mitano ijayo. Hata hivyo, kwa kuchambua vipaumbele vya ILANI zilizopita, na hasa vya Chama Tawala (CCM), yapo mapungufu kadhaa ya makusudi yanayoonekana: Mathalani, Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Chato haukuleta tija kwa uchumi wa taifa hili kwa kipindi husika, na pesa zile zingeelekezwa kuboresha Uwanja wa KIA au ule wa Mwanza, pengine leo hii Soko la Utalii nchini lingekuwa limeimarika zaidi na kutoa ushindani kwa nchi jirani ya Kenya. Ni dhahiri, kila Awamu inapoingia madarakani, inakuja na vipaumbele vya makusudi kupendelea maeneo anakotokea Rais: Mfano – Chato (Awamu ya Tano), Kizimkazi-Zanzibar (Awamu ya Sita) n.k.

NINI KIFANYIKE?

Mwaka huu 2025 - Ilani ya chama chochote cha siasa lazima ijielekeze kuinua Maendeleo ya Uchumi-tegemezi kwa mikoa husika. Mfano: Mikoa inayotegemea zao la biashara kama Korosho, Kahawa n.k; au Mikoa inayotegemea Mazao ya Chakula (parachichi, nyanya, ndizi, mpunga n.k) sharti ILANI iwazingatie.

Aidha, Mikoa ya Kaskazini (Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Manyara) asilimia kubwa imejikuta haipati Maendeleo tena kupitia kilimo cha kahawa au mkonge (katani). Badala yake, UTALII, MADINI NA MIFUGO vimebaki kuwa vyanzo vikuu vya uchumi. ILANI ya 2025 lazima ioneshe itaboresha vipi SOKO LA UTALII, kwa kuwavutia watalii wengi zaidi na hivyo kuinua uchumi wa mikoa hii na taifa kwa ujumla. Ni kweli filamu ya “ROYAL TOUR” ilisaidia sana kuutangaza utalii wa Tanzania, lakini miundo mbinu ya kumshawishi mtalii kutembelea Tanzania miaka ijayo sharti iboreshwe kwa sababu zifuatazo:-

Kiuhalisia Uwanja wa Ndege wa KIA ulijengwa kukuza utalii nchini lakini kwa sasa umetelekezwa, na badala yake kipaumbele kiliwekwa Uwanja wa Chato na Zanzibar. Mathalani, kwa sasa wale mliofika Zanzibar mnajionea “Abeid Kaume International Airport” inavyopendeza. Lakini, ukija KIA ni kama vile kumtembelea mgonjwa wa ICU. Kwa nini? Sababu ni huu ubaguzi ulioanzia Awamu ya Tano (JPM) wa kuitaka mikoa ya kaskazini itulie kwanza hadi mikoa mingine nchini itakapojengeka!!!

Leo hii Treni za Umeme na SGR toka DSM- Dodoma imeifanya mikoa inayopitiwa na usafiri huu kuonekana ya kisasa zaidi na kuwa mbali kimaendeleo tofauti na mikoa mingine. Ukifuatilia Mijadala Mitandaoni ya Wadau wa sekta ya utalii utajionea jinsi ambavyo pamoja na juhudi za filamu ya “ROYAL TOUR” lakini bado ukosefu wa treni za kutokea KIA kwenda Arusha au Moshi kunafanya watalii kupungua nchini /au kwenda nchi jirani.

USHAURI WETU: Vyama Vya Siasa (iwe CCM au Vyama Pinzani) sharti ILANI zao kwa 2025 zizungumzie mikakati kwa miaka mitano ijayo ya namna ya kuboresha Uwanja wa Ndege wa KIA na ujenzi wa SGR ya Umeme kuunganisha mikoa ya kaskazini. Hatua hii itakwenda sambamba na mpango mkakati wa kuboresha miundo-mbinu ya Uwanja wa Ndege wa KIA ili kuwa kweli wa kisasa na Kimataifa. Hata kama serikali ya Tanzania haina Uwezo wa kugharamia yote haya, ni budi iruhusu Sekta binafsi (kwa mfumo wa PPP) kufanya ujenzi huu na kuendesha treni hiyo, kwa sababu faida zake zipo wazi. Ni dhahiri, sekta binafsi ikishirikiana na wadau wa ndani na nje haitoshindwa kujenga kilometa 80 za SGR kutoka Moshi hadi Arusha kupitia Uwanja wa Ndege wa KIA (kwa Awamu ya kwanza). Awamu ya Pili ya ujenzi wa SGR ya Mikoa ya Kaskazini itaunganisha Moshi na Bandari ya Jiji la Tanga kwa miaka ijayo, na hivyo kuchochea maendeleo.

FAIDA ZAKE: Endapo utekelezaji wa mradi huu utafanyika kama tunavyoshauri, Usafiri wa Mabasi kutoka na kwenda mikoani utaanzia Moshi Mjini na kuishia Moshi Mjini. Ins maanisha kuwa, Abiria wafikapo Moshi Mjini watapanda treni ya Umeme kwenda Arusha, kama ambavyo Abiria na wasafiri watokao mikoa mingine wafikapo Arusha watalazimika pia kutumia treni ya SGR kuja Moshi. Aidha, yatakuwepo mabehewa maalumu ya kubeba watalii wanaoshuka kwa ndege KIA /au wanaowahi usafiri wa ndege kupitia Uwanja wa Ndege KIA. Kwa hiyo, treni hii haitarajiwi kukosa abiria / wasafiri wakati wowote ule. Pili, foleni za magari na mabasi zitapungua jijini Arusha, na kulifanya jiji hili kuzidi kivutio cha watalii. Tatu, kutalifanya Jiji la Arusha kulipiku Jiji la Nairobi (Kenya) kwenye soko la utalii. Nne, mzunguko wa fesha na Uchumi wa Mikoa ya Kaskazini vyote vitaanza tena kuimarika, na Wananchi tuishio huku kujiona hatutelekezwi tena kimaendeleo. Tano, wakati na baada ya utekelezaji wa miradi hii, ajira zitapatikana kwa vijana waishio mikoa hii.

MWISHO: Tunatoa wito kwa ILANI za Vyama vya Siasa 2025, kuzingatia Kilio cha Mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania. Kura za Urais na Wabunge kwa mikoa hii minne zitapatikana siyo kwa maneno matupu bali kwa namna gani vyama hivi vitakavyonadi ILANI zao za Uchaguzi 2025 zenye vipaumbele vya SGR ya Kaskazini na Uwanja wa Ndege wa KIA kwa sababu ndivyo vitakavoinua uchumi-utalii uliodorora kwa mikoa yetu hii, kuongeza ajira na hatimaye kufifisha dhana ya ubaguzi ulioanzishwa na Awamu ya Tano kwa mikoa hii kujiona imetelekezwa kwenye Vipaumbele vya Maendeleo vya Kitaifa.

TUNAWASILISHA.

(Wadau wa Maendeleo Tanzania)
 
Anzisheni vita kama M23 muunde jamhuri yenu.
 
Kwa uchaguzi gani uliopo Tanzania hadi uzungumzie habari za ilani?
 
Kwani inafanyiwa vetting na nani?
 
Back
Top Bottom