Mwandwanga
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 3,059
- 1,572
Tarehe mbili mwezi huu nilibahatika kuitembelea shule yangu Ilboru,nilihudhuria pia mahafali ya 20 ya hii shule. Wadau shule yetu bado inafanya vizuri.....vijana bado wanalitunza jina la shule hii iliyotukuka kwa jamii ya Watanzania walio wengi. Mgeni rasmi alikuwa ni Frederic Sumaye ( Waziri mkuu mstaafu wa serikali ya Tz awamu ya tatu ). kwa machache niliyo yaona na kuyasikia nachukua fursa hii kuwatakia afya njema wakati huu wakisubiri mitihan yao ya mwisho katika ELIMU NGAZI YA SEKONDARI.KILA LAKHERI MADOGO...