Ile ngumi haikuwa ya kawaida

Ile ngumi haikuwa ya kawaida

MtotoKautaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2018
Posts
373
Reaction score
895
Nawasalimu kwa jina la Engonga Baltazar.

Mwaka 2017 nipo advance nilitoroka skul nikaenda kukesha kwenye mwenge, napenda sana muziki na nilikuwa na talent ya kucheza na kuimba ila sjui vimepotelea wapi nimebakiza kuimba tu labda.

Kulikuwa na mziki unarindima so mchezo, mida ya saa tano kuelekea saa sita usiku.
Kukawa na mwanamke mmoja kalewa anatembea kwa kuyumba sana sasa akawa anagonga gonga watu.

Kagonga gonga watu akamgonga mlevi mwenzake wa kiume kama hatua moja kutoka nilipokuwa nimesimama.
Yule jamaa Wacha amuamshie popo yule mwanamke, kaanza kumramba vibao hafu watu wanashangalia walevi wenzake na yule jamaa.

Mimi huruma ikaniingia (na huo ndo ulikuwa mwanzo wa matatizo). Huruma ikanijaa nikajikuta namzuia mwamba asiendelee kumpiga yule mwanamke. Jamaa akanipiga kofi kwenye bega la kulia, nikaona so kesi nikarudisha ngumi. Mwamba nilimpiga ngumi kifuani akaanguka chini watu wakajaa zaidi, wenzake na yule mwamba wakanivagaa walikuwa wamelewa sana mwanzo niliweza kuwapiga makonde mm nilikuwa sijagusa pombe kwahyo nikisukuma ngumi inafika kweli kweli.

Niliwalaza chini kama watu wa3 hivi wengine Kwa mitama wengine Kwa ngumi, mlevi ni rahisi sana kumpiga tena sana hasa aliyelewa chakali unajipigia tu. Sasa nimejisahau naenda kumvuta yule dada atoke pale alipokuwa kasimama atokomee zake arudi kwao, wazee nilistukia nimepigwa ngumi moja ya kichwani asee kuna watu wamekomaa.

Nilipopigwa ile ngumi nilijikuta nimenguka chini kichwani nikawa nasikia maumivu makali sana nilijikaza nikajivuta nikaamka nikatoka spidi Kali sana nikaenda mbali kuskilizia maumivu nikarudi skul kesho yake niliamka saa tisa alasiri kichwa kinauma kinoma nikapata dawa nikaoga nikala nikalala tena nikaamka saamoja usiku ndo nikawa na nafuu.

Sikuwahi kurud tena kwenye ishu za kukesha kwenye mwenge na kuingilia ugomvi usonihusu kwasabab ya huruma nikakoma labda awe ni mtu wangu wa karibu na iwe ni uonevu wa nje nje na naona kuna dalili ya kupata kampani hapo ndo ntaingilia la sivyo hapana wazee.
 
Vijana msiingie kwenye ugomvi kama mnajijua hamna nguvu na mbinu za kupambana mtakuja kuacha meno!, hivyo vitu tunaviweza sisi wenye black belt ninauwezo wakukalisha watu watano!, upiganaji unakanuni zake pia ni ujanja binafsi na pia uwe faster kuna baadhi ya mapigo kabla hayajakufikia unatakiwa uyawahi!.

wewe ngumi moja tu ya kisogo ukaanguka hapo kama mtu anakisu anakuwahi anakuchimbua maini!!.
mimi nakupiga mpk ukipelekwa hospitali wanasema ungeletwa jana wakati umepigwa dk tano zilizopita tu!.
 
Vijana msiingie kwenye ugomvi kama mnajijua hamna nguvu na mbinu za kupambana mtakuja kuacha meno!, hivyo vitu tunaviweza sisi wenye black belt ninauwezo wakukalisha watu watano!, upiganaji unakanuni zake pia ni ujanja binafsi na pia uwe faster kuna baadhi ya mapigo kabla hayajakufikia unatakiwa uyawahi!.

wewe ngumi moja tu ya kisogo ukaanguka hapo kama mtu anakisu anakuwahi anakuchimbua maini!!.
mimi nakupiga mpk ukipelekwa hospitali wanasema ungeletwa jana wakati umepigwa dk tano zilizopita tu!.
Ile ngumi nilistukizwa nimemgeukia yule mwanamke jamaa kanivizia kanipigia.
 
kwani uzubae wakati upo kwenye mapambano?, hujui dhaifu moja tu linatosha kupokwa ushindi..??
wewe sema ukweli ulikuwa unaangalia nyash ya huyo dada mlevi!
Mimi nilijua tyr ugomv ushaisha nishashinda
 
Mimi nilijua tyr ugomv ushaisha nishashinda
Kuna jamaa kidogo atolewe meno kwa kuhis ugomvi umeisha akawa anatafuta sendo zake pasipo tahadhari,kajamaa kalimpiga kickfoot ya mdomoni na ngumi za mdomon jamaa alianguka kama mlevi na mdomoni akiwa kajaa damu tayar
 
umenikumbusha sana mbali
mambo ya vilabuni 2001, nimekaa na jamaa yangu ya meli maarufu,jamaa kaja kamwazishia rafiki yangu na ananakozi yamana ....alipigwa nikasikia kilio kikubwa sana .....kwamba ,NIMEPIGIWA na sturi sio ngumi mama nakufaa....
 
Back
Top Bottom