Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
ILEJE: Hoja 38 za tangu 2009 bado hazijajibiwa RC Mgumba ageuka mbogo kwa Baraza la Madiwani.
SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amegeuka mbogo kwenye Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ileje baada ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG kuonyesha Ileje ina Hoja 38 za kiutendaji ambazo bado hazijajibiwa na Halmashauri.
Mkuu wa Mkoa amesema ayo kufuatia Halmashauri ya Ileje kujibu hoja 25 tu Kati ya 63 za zamani ambazo nyingine ni tangu 2009 na kupelekea Halmashauri kwa sasa kuwa na Hoja 60 ambazo hazijajibiwa ikiwa ni pamoja na za zamani.
"Halmashauri itakayovusha hoja ya mwaka uliopita kwangu mimi itakuwa ni ushahidi tosha kuwa Mkurugenzi na watalamu wanaokusaidia wote hamtoshi" Omary Mgumba.
Mkuu wa Mkoa amesema hoja nyingi za Halmashauri ni hoja zilizo ndani ya uwezo wa Mkurugenzi na sio hoja za kisera ambazo zinahitaji Serikali Kuu kuzitatua.
Aidha Mgumba ameeleza kuwa hoja nyingi za kiutendaji ni malipo yamefanyika lakini hakuna risiti, kutofwata taratibu za manunuzi na kutumia fedha nje ya Bajeti.