Uchaguzi 2020 Ilemela, Mwanza: Prof. Lipumba aahidi kuwalipa fidia Wavuvi

Uchaguzi 2020 Ilemela, Mwanza: Prof. Lipumba aahidi kuwalipa fidia Wavuvi

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amewaahidi wavuvi wa eneo la Kayenzendogo wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, kuwa atahakikisha hakuna mvuvi anayechomewa nyavu zake na kila mvuvi aliyenyang'anywa na kuchomewa nyavu atalipwa fidia.

Prof. Lipumba ameyasema hayo wakati akisalimiana na Wavuvi wa Mtaa wa Kayenzendogo wilayani humo, ambapo ameeleza kuwa yeye atakuwa ni rais wa wanyonge na atakapopata ridhaa atawasimamia wavuvi wapate stahiki zao.

Prof. Lipumba adai kuwa hivi karibuni serikali imewanyang'anya na kuwachomea wavuvi wengi nyavu zao na baada ya muda mfupi ikasema nyavu hizo ni halali, jambo ambalo limekuwa likiwasababishia wavuvi wengi hasara na hatimaye kushindwa kuendelea na uvuvi wao.
 
Lipumba huyu huyu Pandikizi la Nyerere na CCM???????????
 
Back
Top Bottom