Ili kelele zipungue kuhusu bandari Serikali ifanye yafuatayo!

Ili kelele zipungue kuhusu bandari Serikali ifanye yafuatayo!

Imma_Magira

Member
Joined
Jan 8, 2022
Posts
19
Reaction score
27
Imeandikwa na Aron Seni (LLB-Mzumbe)

Sote ni mashahidi mpaka sasa kuna mvutano mkali kuhusu Bandari. vyama pinzani, wanasheria na wanaharakati wanadai huu(IGA) ni mkataba wa halali wakati huohuo mawaziri, wabunge, na maofisa wa serikali wanasema huu siyo mkataba Bali ni mkakubaliano tu.

Swali gumu ambalo serikali haijajibu mpaka sasa ni je, kama ni makubaliano ya kawaida Bunge lilipata wapi mamlaka ya kuridhia makubaliano?

Kwasababu katiba ya nchi hii ibara ya 63(3)(e) iko wazi inatamka hivi Bunge Lina mamlaka ya "Kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu jamuhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa. "

Hapo hakuna neno kuridhia makubaliano, Sasa Bunge lilipata wapi mamlaka hiyo?.

Wapo baadhi ya viongozi wanadai katiba ya kiingereza imetamka neno mkakubaliano (agreement), na hii ni kweli kabisa.

ukisoma ibara ya 63(3)(e) ya katiba ya Tanzania iliyochapishwa kiingereza inasema hivi; The parliament may "Deliberate upon and ratify all treaties and agreements to which the united republic is a party and the provisions of which requires ratification."

Sasa iko hivi, Kisheria ukiona lugha mbili zinakinzana. mfano, katiba ya Tanzania iliyoandikwa kiingereza na Ile ya kiswahili endapo Kuna neno au maneno ya Ibara moja yanakinzana katika maana, hapo Kuna moja ndiyo itakayotumika kuamua ugomvi.

Na katika kuamua huamui kwa utashi wako binafsi, unatakiwa kutumia kanuni.

Kanuni inayotumika hapo inaitwa The originalism theory.
Hii kanuni inasema hivi, kama katiba iliyoandikwa na kutafsiriwa kwa lugha nyingine italeta mkanganyiko basi itakayotumika ni Ile yenye lugha iliyotumika kuandikwa kwa katiba mara ya kwanza.

Kwa msingi Huo. Katiba yetu ya kiswahili ndiyo itakayotumika na siyo hiyo ya kiingereza kwasababu Version ya kwanza ya katiba yetu iliandikwa kwa kiswahili.

Hivyo basi ni wajibu wa Bunge kufanya yafuatayo ;
1.Wakiri kuwa walichokiridhia ni mkataba halali na siyo makubaliano.

2. Kama ni makubaliano basi watuonyeshe ni sheria Gani inalipa Bunge mamlaka ya kuridhia makubaliano.


Kwanini wanafumbia macho hoja hii?

Kama watakiri kuwa huu ni mkataba halali basi Kuna mambo Haya watakutana nayo.
1. Mamia ya watanzania waliowaaminisha kuwa huu siyo mkataba watapoteza imani kwa ccm na serikali na hii inaweza kuwa faida(political advantage) kwa upinzani.

2. Hoja itakayobaki kwa upinzani itakuwa ni moja tu, kupinga mkataba na wataachana na mambo ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu agenda ya aidha huu ni mkataba au makubaliano, kwa lugha rahisi wapinzani watapunguziwa kazi ngumu.


Aron seni.
LL.B - Mzumbe.
 
Weka namba za simu ukumbukwe kwenye PDF la Zuhra Yunus
 
Back
Top Bottom