Ili kuboresha elimu, Serikali iachane na mpango wa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti 'grade A'

Ili kuboresha elimu, Serikali iachane na mpango wa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti 'grade A'

Alwatan kamba

Member
Joined
Nov 16, 2020
Posts
70
Reaction score
236
Katika kuboresha sekta ya elimu nchini, ni wakati sahihi wa serikali kupitia wizara ya elimu na tamisemi kuachana na mpango wa kutoa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti almaarufu 'grade A'

Sababu ni hizi,

1. Mafunzo ya ualimu wa 'grade A' hayawaandai walimu hao kuendana na soko la dunia kwenye ajira. Sababu ni kwamba mafunzo wanayopata hayawawezeshi kufanya kazi popote katika dunia ya leo kwani mataifa mengi kwa sasa yameachana na mpango wa kuzalisha walimu wa ngazi ya cheti na hivyo elimu hiyo haitambuliki kidunia.

2. Ualimu ngazi ya cheti 'grade A' unazingatia zaidi mahitaji ya nchi lakini hauzingatii matakwa ya dunia kwani walimu wanaozalishwa kupitia mafunzo hayo huishia tu kufundisha watoto ndani ya nchi na sio vinginevyo.

3. Walimu wengi wa 'grade A' hawakufanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne hivyo wanatakiwa kuboreshwa angalau kwa kiwango cha elimu ya stashahada ili kuwaongezea umahiri zaidi kitaaluma na kuendana na matakwa ya kidunia.

4. Ualimu ngazi ya cheti 'grade A' pia unachangia kufeli kwa wanafunzi. Kutokana na uwepo wa mafunzo haya ya 'grade A' wanafunzi wengi huzembea katika masomo kwa kujua hata wakifanya vibaya kwa kupata ufaulu hafifu wa daraja la nne 'division four' wataenda kusomea ualimu huo.

5. Mafunzo ya 'grade A' pia yanachangia kudharaulika kwa kada ya ualimu na kuonekana kama kada kimbilio la watu waliofeli kwani walimu wengi wanaodahiliwa na kuajiriwa kupitia mafunzo ya ngazi ya cheti huwa na ufaulu wa kawaida sana katika matokeo yao ya kidato cha nne.

Kufuatia sababu hizo na nyingine ambazo si vizuri kuzitaja ni vema sasa mafunzo ya 'grade A' yakafutwa rasmi na wizara ya elimu ikaendelea na mchakato wa kuboresha elimu kwa kuboresha walimu wa 'grade A' walioko kazini angalau wawe na kiwango cha elimu ya stashahada kama ilivyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi 2020-2025.

Kauli mbiu ya sera ya elimu na mafunzo inasema,

" Elimu bora na yenye tija kwa maendeleo ya Taifa inawezekana, wote tutekeleze wajibu wetu"
 
Watanzania mnafikiri ufundishaji unatokana na kiwango kikubwa cha elimu. Ufundishaji ni zaidi ya hicho unachofikiri ndugu. Ufundishaji ni karama, ufundishaji ni utamaduni, ufundishaji ni wito, unaweza ukajaza maprofesa huko shule ya msingi na wasiweze kufundisha.

Yaangalieni Mapito ya zamani, ukaone ukweli uliobebwa na hicho cheti. Usisumbuliwe na neno cheti au hiyo form four ya kufeli ama kufaulu, kaangalie utamaduni mzima na mfumo uliobebwa na hicho cheti, kumbuka kuna waalimu wenye diploma na digrii zenu hizo wameenda huko wamekimbia.
 
Huna information.

FYI Ualimu huendi kama una division four.

Pia kuna kujiendeleza.
 
Mbona vigezo vya kujisomea ualimu vilishabadilishwa upo dunia gani ndugu?
 
Mleta mada acha upotoshaji!

Kwa taarifa yako... Hakuna walimu wanaandaliwa vizuri kama wale wa grade A (na diploma). Tena asilimia kubwa wanascarifice maisha yao ili watoto wetu wafaulu...

Matatizo ya elimu yetu yapo kwenye sera zinazowakatisha walimu tamaa ikiwa ni pamoja na kuchanganya siasa na taaluma. Hali inayoyumbisha mustakabali wa elimu elimu ya vijana wetu!

Tatizo lingine la msingi kabisa ni kutokuwa na chama cha walimu kwa maslahi ya walimu...

Nchi hii vyama vya wafanyakazi ni dhaifu lakini kile cha walimu ni utopolo kabisaaaa!
No wonder idadi ya well trained teachers inazidi kupungua siku hadi siku wengi wakirudi masomoni au kutafuta maisha kivingine!!!
 
Mleta mada acha upotoshaji!
Kwa taarifa yako... Hakuna walimu wanaandaliwa vizuri kama wale wa grade A (na diploma). Tena asilimia kubwa wanascarifice maisha yao ili watoto wetu wafaulu...
Matatizo ya elimu yetu yapo kwenye sera zinazowakatisha walimu tamaa ikiwa ni pamoja na kuchanganya siasa na taaluma hali inayoyumbisha mustakabali wa elimu elimu ya vijana wetu!
Tatizo lingine la msingi kabisa ni kutokuwa chama cha walimu kwa maslahi ya walimu...
Nchi hii vyama vya wafanyakazi ni dhaifu lakini kile cha walimu ni utopolo kabisaaaa!
Well said mkuu
 
Back
Top Bottom