Ili kuboresha Sekta za Kilimo na Mifugo nchini, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Ma-DED watokane na Maafisa Mifugo au Kilimo

Ili kuboresha Sekta za Kilimo na Mifugo nchini, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Ma-DED watokane na Maafisa Mifugo au Kilimo

Kididimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
4,153
Reaction score
3,800
Ni ukweli usiopingika kuwa Ili Uchumi wa Viwanda katika nchi yetu uimarike, ni lazima tutegemee Mali ghafi zaidi zinazotokana na Kilimo na Mifugo.

Hivi sasa uzalishaji wa mazao ya Kilimo hasa yale ya biashara mfano kahawa,pamba, mkonge, na mengineyo umeshuka sana kipindi cha karibuni. Hali kadhalika uboreshaji Mifugo unasuasua Sana hadi majuzi namuona Waziri wa Fedha Dr. Mwigilu Nchemba akiishauri Wizara ya Mifugo mbinu mbalimbali.

Ukichunguza kiini cha yote kwa sehemu kubwa ni usimamizi utendaji mbovu wa sekta hizo hasa ngazi za chini. Wakuu wa Mikoa,Wilaya na MaDED wengi siyo wataalamu wa fani hizo na husubiri ya kuambiwa na approach zao kubwa ni amri zisizo na tija! Mifano ninayo.

Tunao Wataalamu wengi wa Kilimo na Mifugo kutoka Vyuo kama SUA hutaona wakiteuliwa katika maeneo haha,wengi wao naamini wana uwezo mzuri Sana. Na ukitaka kufanya utafiti mdogo,angalia waliofanikiwa kujiajiri wanavyofanikisha miradi yap binafsi.

Kwenye Agroprossesing technology ambayo ndiyo ilipromote kwa kiwango kikubwa chumi za nchi kama Vietnam,Taiwan, hata China haitendewi haijatendewa haki vilivyo hapa nchini kwetu. Na sababu kubwa ni uelewa mdogo hasa wa viongozi tunaowapa dhamana ya kubuni,kuhimiza,kusimamia jamii yetu hasa eneo nililolitaja.

Ni rai yangu uongozi ngazi za juu hasa zenye dhamana na teuzi walione hilo
 
Sio kweli!

Wakuu wa Mikoa, Wilaya na hao ma-DED ni wasimamizi wa Sera ya Taifa katika maeneo husika na kuhakikisha kuwa mambo yoote yanatekekezwa kama ilivyooangwa na Serikali.

Kwasababu wakuu wa mikoa, wilaya na ma-DED ni viongozi basi kazi yao kuwasimamia watendaji woote waliochini yao, na sio kwamba wao wanatakuwa wazifanye hizo kazi la hasha!

Kwa maana hivyo basi, kinachotakiwa hapo ni Kiongozi ambae atavaa uthubutu wa kusimamia hizo sera na watu walio chini yake kwa uthubutu kabisa na SIO lazima wawekwe wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya ba ma-DED wanaotokana na maafisa kilimo, hiyo hapana!!!. Lakini ikitokea Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyeteuliwa ana background ya kilimo it will be okay lakini haitaku-guarantee kuwa ndo atakuwa ni kiongozi mzuri.

Ndio maana debate inayoendelea sasa hivi ktk nchi hii ni kujaribu kuwaweka wenye fani za utawala/uongozi wa watu -public administration, uongozi wa biashara-business administration na uchumi kuongoza; Mikoa, Wilaya, Halmashauli, hopitali za mikoa/rufaa/wilaya, shirika la umeme Tanesco n.k

Asante!
 
Nipe sababu ya Msingi ni kwa nini hatukipi Kilimo au Mifugo kama kipaumbele kuelekea Uchumi wa Viwanda?
 
Tafuteni masoko ya mazao yetu acheni longolongo nyingi. Sasa mtu kalima kapata mazao yake tani kadhaa then kakosa soko la mazao yake,, kwa sababu ya kuzuia kuuza mazao fulani nje ya nchi Sasa unategemea huyo mtu msimu ujao aongeze mashamba au apunguze? Nenda hapo morogoro kiwanda cha mtibwa kawaulize wakazi wa pale kwann wakulima wa nje( outgrowers) hawalimi miwa kama ilivyokuwa zamani ukipata majibu ndio utashangaa Mambo yanavyoenda.
 
Wanafunzi wa vyuo vya kilimo hawatumiwi ipasavyo. Kila kijiji kilitakiwa kuwa na nyumba kwaajili ya wanafunzi. Kianzia wa afya hata wakilimo wanaweza kufikia. Kila mwanafunzi akitumia miezi mitatu kwa mwaka vijijini na kupata evaluations za wanakijiji kuhusu ufundishaji wake wa kilimo.
 
Wanafunzi wa vyuo vya kilimo hawatumiwi ipasavyo. Kila kijiji kilitakiwa kuwa na nyumba kwaajili ya wanafunzi. Kianzia wa afya hata wakilimo wanaweza kufikia. Kila mwanafunzi akitumia miezi mitatu kwa mwaka vijijini na kupata evaluations za wanakijiji kuhusu ufundishaji wake wa kilimo.
Sifa ya kuwa DC au RC ni kuwa kada wa CCM au uvccm.
 
Back
Top Bottom