Ili Kuchochea Kilimo, Serikali itoe ruzuku kwenye nafaka za kuuza nje

Ili Kuchochea Kilimo, Serikali itoe ruzuku kwenye nafaka za kuuza nje

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Nakumbuka miaka ya nyuma wakati serikali ikinunua mahindi, ilikuwa ukipita njia ya kati, kuanzia pwani mpaka singida yalikuwa mashamba ya mahindi.

Baada ya Serikali kusua sua katika kununua mahindi, mashamba hayo yamepotea.

Mbali na serikali kutoa ruzuku kwenye mbolea bado mashamba haya hayajarejea.

Mimi naamini Tanzania tunaouwezo wa kuwa wauza nafaka wakubwa barani afrika.

Ni wakati wa serikali kuweka ruzuku kwenye nafaka za kuuza nje, yaani serikali inunue nafaka kutoka kwa wakulima na kuziuza nje katika bara la afrika hata kwa bei pungu na walinunulia kwa mkulima.

Tuweke malengo ya kufikia mwaka 2030 tuwe na uwezo wa kuuza tani milioni 30 za nafaka nje ya nchi.

Ni lazima tuanze kwa kuwekeza na uwekezaji sahihi ni kuwafahamisha wanunuzi wa chakula kote barani afrika kuwa Tanzania watapata nafaka kwa bei nafuu.

Mfano tunaweza kununua mahindi kwa 500 kwa kilo na tukawauzia wanunuzi wa nje kwa 500 hiyo hiyo ili ruzuke iwe ni gharama za logistics n.k au tukauza kwa bei pungufu na hiyo kutoka kwenye maghala yetu.

Faida tutakayoipata katika nchi yetu tangu mwaka wa kwanza ni zaidi ya ruzuku tutakayoiweka.

Na kwa mazingira mazuri ya kilimo tuliyonayo, kilimo kinaweza kuwa ndicho chanzo kikubwa cha mapato ndani ya mda mfupi.

Fikiria tukiuza tani milioni 20 za mahindi kwa kila kilo moja 400 = trilioni 8, tukauza tani milioni 10 za nafaka nyingine kwa bei ya 1500 = trilioni 15

Jumla utapata trilioni 23 kwa mwaka.

Je, hii si sawa na fedha yote inayokusanywa na TRA kwa mwaka?

Haya mambo yanawezekana, ikiwezekana tuleteeni kodi ya kuendeleza kilimo na strategy ya kwanza iwe ni kuongeza soko la nje.

Zamani tulihubiriana kuweka juhudi kujitosheleza na sasa tangu miaka ya elfu mbili na kumi na kitu tumeshajisheleza kwa more than 100%

Fungueni masoko ya nje na siyo kuedelea na akili zilezile za kuchochea uzalishaji wakati tumejifungia tunalishana wenyewe. mkono wa serikali uende kwenye kufungua masoko ya kimataifa na hiyo ni kuwaahidi kupata chakula kwa bei nafuu kutoka Tz.

Nafaka ni rahisi katika handling na hivyo tuweke msukumo kwenye nafaka na hizo zitafungua masoko ya kilimo kwa mazao mengine.
 
Pendekezo zuri mkuu, well wasimamizi kama wanaona lina tija walipitishe
 
Back
Top Bottom