KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Kwako
Rais wa JMT Mhe.Samia Suluhu Hassan
Waziri wa biashara Dkt. Suleiman Jaffo
Nawasalimu kwa jina la JMT,
Awali ya yote nachukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na huruma kwa kutujalia kufika muda na wakati huu tukiwa wazima wa afya na kujaliwa amani na usalama wa kutosha.
Pia, nachukua nafasi hii kukupongeza Mhe.Rais kwa uongozi ulio Bora na wenye kuacha alama ya kudumu kwa Taifa letu.
Mhe. Rais, mara kwa mara umegusia suala la wafanyabiashara kuficha stoo zao na kupelekea upotovu wa mapato na siku ya Jana umegusia suala Hilo ulipokutana kwa ajili ya chakula Cha pamoja na waliosaidia kwenye zoezi la uokoaji kufuatia kuporomoka kwa jengo kariakoo lililozidishiwa mzigo kuliko uwezo wake.
Ni ukweli usiopingika kuwa Kuna upotevu mkubwa wa mapato Kariakoo kutokana na kukosekana kwa udhibiti wa kutosha na ili pawepo na udhibiti mkubwa mhe.Rais nina nina ushauri, maoni na mapendekezo yafuatayo:
Kwanza, Kariakoo ibomolewe na kujengwa upya. Hali ya upotevu wa mapato Kariakoo itaendelea kama kusipokuwa na kupafanya upya na hali ya sasa itaendelea. Zaidi, pasipo kujenga upya basi inawezekana zikatumika gharama kubwa kufuatilia maghala ya maficho ambayo yanahifadhi bidhaa kimagendo bila kulipia Kodi.
Pili, Kariakoo ifanywe SPECIAL BUSINESS zone na itambulike hivyo. Baada ya kuibomoa kariakoo kariakoo ijengwe kisasa. Kuwe na eneo ambalo magari ya kuingiza bidhaa kwa wafanyabiashara yanakaa na taratibu za forodha kufuatia yaani kwa kifupi kuwe na eneo la FORODHA.
Tatu, kila ambacho kitakuwa kinaingia kariakoo kiingizwe kwenye mfumo. Kupitia kituo Cha FORODHA kila ambacho kitachukuliwa na wafanyabiashara kitaingizwa kwenye mifumo yao na hapo kutakuwa na udhibiti mkubwa wa vinavyoingia kwa kuwa kila kitu kitakuwa kwenye mfumo basi itakuwa ni rahisi kudhibiti utokaji wa bidhaa hizo kwa kutumia risiti na hapo serikali itadhibiti upotevu wa mapato.
Nne, kwa kuwa kutakuwa na udhibiti wa bidhaa kuingia, basi kariakoo ikijengwa upya kutakuwa na udhibiti wa bidhaa kutoka. Kuwe na ukaguzi wa risiti wa maeneo ya kutokea.
Tano, yaani kwa kifupi tufanye kariakoo kuwa SUPERMARKET KUBWA ambayo kila kinachofanyika kunakuwa na udhibiti wa kutosha. Kuingiza mizigo kuwe na udhibiti, kutoa mizigo kuwe na udhibiti kama inavyofanyika kwenye SUPERMARKETS.
Sita, tusiishie kwa kariakoo tu hata masoko mengine ya kimkakati pawe hivi na tukianza na soko la Jangwani ambalo mhe.Rais umesema litajengwa nafikiri utekelezaji utakuwa wa kiwango na kusaidia serikali kukusanya mapato mengi.
Naomba kuwasilisha
Ahsante