SoC04 Ili kufikia Tanzania tuitakayo tunatakiwa kushiriki katika miundombinu bora ya kuijenga Tanzania yetu tuitakayo

SoC04 Ili kufikia Tanzania tuitakayo tunatakiwa kushiriki katika miundombinu bora ya kuijenga Tanzania yetu tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

juwairiya othman

New Member
Joined
Jun 1, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Ili kufikia malengo ya kufanikisha Tanzania tuitakayo tukianzia kwenye suala la mazingira

Tanzania ni nchi ambayo inae mazingira bora inae mazingira mazuri sana lakini tukija baadhi ya maeneo mazingira yake yanakuwa yako katika hali tatanishi ambapo unakuta takataka haziwekwi katika sehemu sahihi Hadi kufikia Hali ya mlipuko wa magonjwa kama vile kipindupindu hivyo basi ili kufikia Tanzania tuitakayo inabidi katika Kila mtaa au Kijiji viongozi wakae vikao na wananchi wao kuwashauri kuhusu kutunza mazingira ambapo ILI kuepukana na magonjwa.

Katika Kila mtaa kunatakiwa wananchi washiriki katika kuchangia pesa kidogo kwaajili ya kununua sehemu maalumu za kuhifadhia taka kama vile dustbin kwasababu ni majukumu yetu sisi kama watanzania kuhifadhi na kutunza mazingira yetu endapo tutashiriki vizuri katika kuchangia pesa kidogo kwaajili ya sehemu ya kuhifadhia taka.

61qAYz1TI9L._AC_UF1000,1000_QL80_.jpg

Dustbin ni sehemu nzuri kabisa ya kuhifadhia taka ILI zisizagae katika mazingira yetu pia na sisi tunatakiwa kuwahimiza watu wengine kutunza mazingira na kuhifadhia kwenye dustbin.

Utunzaji wa mazingira utatusaidia katika kufikia Tanzania tuitakayo kwasababu ILI kufikia katika hatua fulani tunatakiwa tuanze katika hatua za chini ILI baada ya muda tunafikia katika hatua kubwa hivyo basi hatua ndogo ni kama utunzaji wa mazingira na afya pia kama mazingira yatakua ni masafi pia na watu wanatakiwa wawe na afya bora kwasababu watu wakiwa na afya bora watasaidia katika utunzaji wa mazingira.

Baada ya kuanza na hatua ndogo tutapiga hatua ndogo ndogo ndio umuhimu wa kupiga hatua ndogo ndogo mwisho wa siku tunafika kwenye mafanikio tunayoyahitaji.

Successful.jpg


Lakini kama tutaanza kwa kutaka kupiga hatua kubwa kufanikiwa itakua ni ngumu kwasababu mfano mdogo ni pale mtu anapopanda ngazi. Ngazi hatua zake hua ni ndogo ndogo mpaka inafikia hatua mtu amefika sehemu anayotaka kwa kupiga hatua ndogo ndogo lakini kama tutataka kuanza kupiga hatua kubwa itakua shida mfano hii picha hapa chini... Hii picha inaonesha ugumu wa kuanza na hatua kubwa ndo maana tunatakiwa tuanze na hatua ndogo ndogo kwanza halafu ndo tufikie ile hatua tuitakayo.


5db44d49bac52843cc6d76fa9e1695b7(0)_1.jpg
Katika ujenzi wa taifa letu au ujenzi wa nchi yetu tunatakiwa chakwanza kabisa tuweze kutunza rasilimali zetu na miundombinu yetu ILI iwe bora zaid tuje kwenye suala la upandaji miti.

Baadhi ya maeneo wamekua wakikata miti hovyo na kutumia katika biashara zao Sasa Hii Hali unaweza kusababisha mmomonyoko wa udongo katika maeneo Sasa Hii huleta athari kubwa zaidi kwenye nchi kwasababu inaleta muonekano mbaya katika nchi mfano wa hii picha ambapo wamekata miti hovyo inaleta muonekano m'baya katika nchi yetu.

fcc2720edceff5afcd52ecc65da1256d4c834479.png


Sasa sisi kama wananchi tutakua na ushirikiano mzuri wa kupanda miti italeta muonekano mzuri kwenye nchi yetu na italeta faida nyingi sanaa katika nchi yetu italeta muonekano mzuri kwenye taifa letu italeta hewa safi katika nchi yetu na itakua pia sehemu ya utaliii kama kutakua na mazingira mazuri na masafi pia yenye miti mingi na mizuri pia kama picha ifuatayo hapo chini.

175-1751679_jungle-rain-wallpapers-top-free-jungle-rain-backgrounds-848x450.jpg
Muonekano wa picha hiyo hapo unaonekana ni mzuri kwasababu ni kitu asilia na kinachotunzwa kwahivyo basi tunatakiwa tushirikiane kupanda miti na kumwagilia pia.

Tukifuatia kwenye upande wa vyanzo vya maji vyanzo vya maji
ni muhimu sanaa kwenye maisha ya binaadam lakini wengi wao wamekua hawavitunzi vyanzo vya maji unakuta mtu anatupa taka labda kwenye ziwa n.k Sasa Hii inaathiri vitu vingi sanaa hasa kwenye upande wa afya zetu unakuta watu wanafua kwenye vyanzo vya maji au wanajisadia kwasababu asilimia kubwa sana ya watu wa Tanzania hawana elimu Sasa kwa kushirikiana vizuri na Serikali tunaweza kuwaelimisha watu wasio na uelewa wa kutunza mazingira na baada ya kuwapa elimu tunaweza kutatua tatizo la uchafuzi wa vyanzo vya maji asilimia kubwa vyanzo vya maji huchafuliwa sana Hadi kupelekea mlipuko wa magonjwa tufuatilie kielelezo ambacho kinatuonesha uchafuzi wa vyanzo vya maji

uchafuzijpg-768x470.jpg
ila kama

Tutashirikiana vizuri katika kuijenga Tanzania tuitakayo lazima tutavitunza vyanzo vyetu vya maji na kua visafi na visivyo na athari zozote kama kielelezo kifuatacho

Mto-Rufiji.jpeg
Kama tukiwaelimisha watu kuhusu utunzaji wa mazingira basi Kila kitu kitakua sawa kielelezo hiki kinaonekana ni kisafi kwa kua wanakisimamia vizuri na wanajua umuhimu wa vyanzo vya maji kama tutaanza na kuwapa elimu ya mazingira basi mazingira yatakua ni mazuri sanaa.

Tufuatie kwenye maji yanayotuama katika barabara na mitaani katika nchii hii ya tanzania asilimia kubwa Sana katika mikoa yetu ya hapa tanzania maeneo mengi sana wanajua hawatilii maanani suala la maji yaliyotuama barabarani na mitaani watu huchukulia ni kitu cha kawaidaa Sana ambapo maji haya yaliyotuama husababisha athari nyingi Sana na kubwa pia kama magonjwa chipukizi kama kipindupindu n.k ambapo magonjwa haya husababisha tunawapoteza watu wengi sanaa lakini kama elimu tukiwapatia raia wakajua umuhimu wa kutunza mazingira na umuhimu wa afya zetu pia basi mazingira yatakua masafi na yanavutia pia tuangalie kielelezo kifuatacho cha majia yaliyotuama mitaani.

1.JPG


Kwa macho ya kawaida kama hatutawapatia elimu wakazi watanzania tunaweza kupoteza idadi kubwa ya watu lakini kama tukiwapatia elimu ya mazingira usafi na kuhifadhi taka basi tungepata ushirikiano mkubwa zaid wa kujenga mitaro bora yenye kupitisha maji yanayotuama tuangalie kielelezo kifuatacho kinachotuonesha mitaro bora ya kupitisha maji machafu yaliyotuama.

IMG_9594.JPG
Mitaro hii itatusaidia kupunguza maji machafu yaliyotuama ambayo yanaleta athari kubwa zaidi katika jamii zetu tuweze kushirikiana na raia wenzetu na kuwapa elimu ya mazingira bora na masafi ILI kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

Hivyo basi ili kufikia malengo ya Tanzania tuitakayo tunatakiwa tuanze katika hatua ndogo ndogo kama usafi wa mazingira na kuwapa watu elimu ya mazingira na afya kwasababu kama mazingira ni masafi na pia watu wanae afya njema tutashirikiana vyema zaidi kwenye kuijenga tanzania tuitakayo.
Ahsante sana.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom