Ili kuhalalisha Ubunge wa Halima Mdee na wenzake, Bunge lirekebishe kifungu cha sheria

Ili kuhalalisha Ubunge wa Halima Mdee na wenzake, Bunge lirekebishe kifungu cha sheria

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Wabunge 19 waliofukuzwa na chama chao CHADEMA kwa mujibu wa Katiba walistahili kuondolewa Bungeni kutokana na kupoteza sifa kwani ili uwe Mbunge ni pamoja na kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

Kwa kuwa Spika pamoja na Serikali inawatambua kuwa ni wabunge halali licha ya kufukuzwa na chama chao nashauri Serikali ipeleke marekebisho ya sheria ya huwa hata Usipokuwa Mwanachama wa chama cha siasa unaweza kuwa Mbunge, kwa Marekebisho hayo Halima na wenzake watakuwa Wabunge halali kama Spika anavyotaka.
 
Wafanye hivyo kwa kubadilisha sheria ya mikutano ya siasa pia ili tusiendelee kutafutana ubaya bila sababu, haiwezekani yule anaepigania haki yake akaitwa "mleta vichokochoko" hiki kitendo kinaonesha hii nchi sasa haina sheria, sheria zilizopo ni vile watawala wanavyotaka mambo yaende according to their wish.
 
SiSiEM ni Ile Ile....Yenye Kutozingatia utawala wa Sheria na kuvunja Katiba. Wanachaguliwa Kwa Mwongozo wa Katiba na Sheria ila wakishamaliza Kuapa Wanazikanyaga Sheria na Katiba...Tufanyeje ili CCM ijue Nchi hii ni Yetu wote. Tutaendelea Kulalamika Hadi lini??
 
Wabunge 19 Waliofukuzwa na Chama Chao CHADEMA kwa Mujibu Wa Katiba Walistahili Kuondolewa Bungeni kutokana na kupoteza sifa kwani ili Uwe Mbunge ni Pamoja na Kuwa Mwanachama Wa Chama cha Siasa.

Kwa kuwa Spika pamoja na Serikali inawatambua kuwa ni wabunge halali licha ya kufukuzwa na chama chao nashauri Serikali ipeleke marekebisho ya sheria ya Kuwa Hata Usipokuwa Mwanachama Wa Chama cha siasa unaweza kuwa Mbunge, Kwa Marekebisho hayo Halima na Wenzake Watakuwa Wabunge Halali kama Spika anavyotaka.
Mkuu hilo suala sio la Kisheria. Ni la kikatiba. Kubadili sheria ni rahisi ila Katiba sio rahisi kama unavyodhani. Ni mchakato mrefu wenye maoni mengi.
 
CCM na Haki ni sawa na maji na mafuta.Tudai Haki ya Katiba Bora.
 
Mkuu hilo suala sio la Kisheria. Ni la kikatiba. Kubadili sheria ni rahisi ila Katiba sio rahisi kama unavyodhani. Ni mchakato mrefu wenye maoni mengi.
Kama ni la KIKATIBA basi Warekebishe Vifungu ndani ya Katiba Uwezo huo Wanao Kama Walivyoweza Kuwaapisha na kuwalipa Mishahara huku Wakijua ni Wabunge Waliofukuzwa na hawa Chama wakati Sifa ya Mbunge lazima Awe Mwanachama wa Chama cha Siasa
 
Kwa kigezo cha kuwa ni wabunge wa CHADEMA.
Tumia Akili usilete Utoto au ndio huyu
JamiiForums-981320052.jpg
 
Kama ni la KIKATIBA basi Warekebishe Vifungu ndani ya Katiba Uwezo huo Wanao Kama Walivyoweza Kuwaapisha na kuwalipa Mishahara huku Wakijua ni Wabunge Waliofukuzwa na hawa Chama wakati Sifa ya Mbunge lazima Awe Mwanachama wa Chama cha Siasa
Sasa mkuu unadhani Mh. Spija atajaribu kuruhusu hiyo hoja?
 
Wabunge 19 waliofukuzwa na chama chao CHADEMA kwa mujibu wa Katiba walistahili kuondolewa Bungeni kutokana na kupoteza sifa kwani ili uwe Mbunge ni pamoja na kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

Kwa kuwa Spika pamoja na Serikali inawatambua kuwa ni wabunge halali licha ya kufukuzwa na chama chao nashauri Serikali ipeleke marekebisho ya sheria ya huwa hata Usipokuwa Mwanachama wa chama cha siasa unaweza kuwa Mbunge, kwa Marekebisho hayo Halima na wenzake watakuwa Wabunge halali kama Spika anavyotaka.
Ndiyo; ila hawathubutu kwa kuwa hicho kitakuwa kisu cha kuwachinja wao.
 
Back
Top Bottom