ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,553
Si tu kuwa kutapatikana mwelekeo wa wapi tunaenda katika football world, bali pia kutafungua vichwa na kuleta kujitambua kwa mamilioni ya Watanzania ambao mawazo yao na upeo wao katika uelewa wa mpira wa miguu duniani ni Simba na Yanga.
Hivi vilabu vikiendelewa kuachiwa na serikali vitazidi kuharibu vizazi na vizazi. Miaka nenda rudi watu watakua wakibishana, kurushiana vijembe, kula pesa kwa kujificha kwenye kivuli cha uongozi, lakini maendeleo yeyote kimataifa hakuna.
Leo hii vilabu vichanga mfano Namungo, Gwambina vinatikisa timu hizi mbili kongwe zilizoanzishwa toka 1930's. Miaka yote hiyo ukiangalia havijafanya makubwa kwa miongo mingi lakini pia hata viwanja hazina. Kazi ni migogoro, kufukuza walimu na ubadhirifu.
Serikali iamke. Hivi vilabu ni sumu kwa wachezaji wachipukiao hapa nchini,ni sumu kwa vilabu vingine vichanga, ni sumu kwa maendeleo ya mpira wa miguu, zifutwe na tubaki na timu zingine kuliko kuendelea na timu ambazo zimekua kama dini bila vision, mbaya zaidi zinawaathiri Watanzania wengi kiakili.
Sent using Jamii Forums mobile app