kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Vijidudu/virusi vya corona vinaweza kuishi kwa muda kadhaa kwenye nguo, ngozi ya mwili, vitasa vya milango na maeneo kadhaa mbalimbali kama vile simu, samani, viti, mikoba, kalamu, madaftari, nk. Ndio maana tunasema tunawe mikono mara kwa mara na kuepuka kujishikashika usoni, puani na mdomoni ili kupunguza uwezekano wa kuvihamisha vijidudu kutoka hapo vilipo kwenda kwenye njia zetu za hewa kwa kupitia mikono yetu sisi wenyewe.
Kwakua vijidudu vya maradhi vinaweza kuishi kwenye vitu mbalimbali vinavyotuzunguuka vikiwemo nguo, vitu na kwenye ngozi zetu,hivyo ni vema uwe unapunguza uwezekano wa kukutana navyo kwa kupunguza vitu tunavyoambatana navyo kila siku.
Punguza kuvaa nguo na vitu vingi visivyo lazima kama vile skafu, kofia, tai, makoti, vikoi, bangili, saa, mabegi, mikoba, simu nyingi za mkononi ili kupunguza vitu ambavyo vijidudu vinaweza kujificha na kukutana navyo huko, yaani kuepuka kuvi contaminate.
Kama sio lazima epuka kutembea na vitu na nguo nyingi zisizo za lazima.