Ili kukabiliana na tatizo la ajira serikali inabidi iruhusu uuzaji wa mazao nje ya nchi

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Vijana na watu wengi hawapendi kulima kwa sababu mbili. Kwanza ni kukosekana kwa masoko ya uhakika wa mazao ya kilimo na bei kuwa ya chini. haya yote yanasababishwa na serikali kuzuia watu kuuza mazao nje ya nchi wakati uzalishaji na potential ya kuzalisha ni kubwa sana.

Ninaweza sema Tanzani kuna deflation ya bei ya chakula. Deflation ina madhara yake, kwanza inapunguza uzalishaji na kusababisha unemployment. Deflation ya chakula inanufaisha wachache na kuumiza wakulima ambao ndiyo wengi. Imekuwa nafuu kununua kuliko kulima. Hii inamaanisha wakulima huzalisha kwa hasara.

Je ni kweli kufungua mipaka kutaleta njaa?. Nchi yetu inazalisha ziada ya msosi pia naamini inaweza kuzalisha hata mara mia ya kiwango cha sasa kwa ardhi na maji tuliyo nayo. Hivyo kufungua mipaka kutaongeza uwekezaji kwenye kilimo, kutaongeza uzalishaji na matokeo yake ajira kuongezeka. Pia vijana wengi wataanza kujiajiri na kilimo maana kitakuwa kinalipa.

Sasa kwanini wanazuia? Kama tunavyojua mabadiliko ya kisiasa huanziaga mijini. Serikali kwa kuona hilo huamua kuwapumbaza watu wa mjini kwa kuhakikisha bei ya chakula ipo chini na njia moja ni kufunga mipaka. Wanafanya hivyo kwa expense ya 80% ya watanzania. Hata hivyo watu wengiwamjini pia hulima au wangependa kuwekeza kwenye kilimo. So hii strategy inatutafuna sote.

Ili kukabiliana na ajira serikali inatakiwa iruhusu uuzaji wa mazao nje, itatengeneza ajira nyingi sana. Na siyo kufungua kinafiki. Kufungua harafu kuweka kodi ya kuexport kubwa ili kudiscourage watu.
 
kamata "like" mkuu. nitarejea baadaye na mchango wangu ingawa sentensi yako ya kwanza inanitatiza hapo kwenye Vijana kutopenda kilimo - ni hawa hawa Vijana wanaoregeza suruali/kaptura, wanaovaa suruali-mbano na kucha, kuchwa earphones masikioni unaowaongelea hapa?
 
kuna wasiojitambua. ila kuna wale walikuwa wanalima na baada ya kuona kilimo hakilipi wakaamua kwenda mjini kuuza socks, karanga, kuendesha bodaboda, kuuza korosho na mahindi. hawa ni wengi sana.
 

Huu uzi umeuanzisha leo? Uko sahihi lakini kila kitu kiko outdated Wizara ya Kilimo haina sera hiyo siku hizi ni ruksa kuuza mazao mahali popote wakati wowote.... Hilo angalau Malima alilivalia njuga
2. Hatupati masoko ya uhakika kwa sababu tunalima kwanza ndio tunaenda kutafuta masoko dunia ilishahama huko yaani hiyo ni sawa na kuuza nguo za mtumba soko la ulaya. Dunia ya leo walaji ndio wanao dictate aina na viwango vya bidhaa.. Tuseme tu kuwa masoko ya bidhaa za kilimo yapo mengi sana kama serikali ingeamua kuyatafuta... Una habari kuwa china ni wanunuaji wakubwa wa mahindi duniani? Soko la mboga na matunda EU Africa tunachangia less than 5% bado ipo potential kubwa. Wachumi wa nchi hii na viongozi wao wa kisiasa wanaendaga ziara kushangaa maghorofa tu
 
Si kweli kwamba imeruhusu. Mwaka 2014 serikali imeruhusu uuzwaji wa mazao nje kama mwezi wa nane. Hapa ni baada ya kuona haitaweza kununua mazao yote. Sasa mtu akilima anakuwa hajui kama serikali itaruhusu au la, kulima inakuwa kamari. Kama ulivyosema wakulima na exporters wanatakiwa kujua watakouza hara kabla ya kulima
 
hakuna jipya katika hii nchi , nililima heka karibu kumi za mahindi , kamtaji kangu kakafia huko, mbolea elfu 60 , wakati gunia la mahindi alfu 15 kweli jamani , nani arudi kwenye kilimo, bora nigange njaa na kadegree kangu hapa town
 
Dunia ya leo kitu kinachoitwa taarifa ni cha thamani sana, pata picha mkulima miaka nenda na kurudi wanalima ila madalali wanaendelea kuwalalia, kwanini?? Kwasababu madalali wana taarifa za masoko ila yule mkulima wa kijijini hajui kitu kama hiko. Kwamfano mkulima anaweza kuuza kilo moja ya ufuta kwa 2000 ila dalali akija mjini anauza 4000. Super profit!!!

Wakulima waungane ili wawe na sauti moja serikalini na kwenye mabaraza ya kutunga sheria na sera, hii itasaidia interests zao kuingia moja kwa moja serikalini. Mwisho wa siku sera zozote kuhusu kilimo hazipitishwi serikalini bila kuongea na wakulima. Leo hii tunaingiza hadi mayai, sukari wakati hivi vitu vinazalishwa tanzania. Kwa mkulima mmojammoja inakuwa ngumu kupambana na hii serikali dhalimu ila kwa umoja inawezekana.

Kwenye umoja wa wakulima kwenye vikundi itawasaidia kupata mikopo nafuu, pembejeo za kisasa, kujenga viwanda vidogo kwa ajili ya kuongeza thamani mazao yao na hata kukusanya mzigo mkubwa kwenda kuiza nje ya nchi.

Pia wananchi waanze kujifunza kulima kisasa kutoa mazao mengi kwenye eneo dogo.

Na serikali ipige marufuku uuzwaji wa mazao ghafi nje ya nchi, zaidi isisitize wakulima kuongeza thamani mazao yao ili wazidi kuongeza kipato.
 

Hakuna zuio la kuuza nafaka nje ya nchi last yr, Wzr mwenye dhamana ya kufanya hivyo ni wzr wa kilimo na abaruhusiwa kuzuia pale tu kama kuna shortage ya chakula nchini, ulisikia tangazo la serikali?
Lakini pia wadau wakaleta mawazo na lots of thinking kuna wakulima wengi biashara ya mahindi ndio kuu, kwa nini umpe adhabu ya kutouza soko zuri kwa expense ya wavivu wachache wasiotaka kujishughulisha?? Ndio serikali ikasema hakuna haja ya kuwa na zuio la namna hii kwa ulimwengu wa leo
Kinachowasumbua ni wakuu wa mikoa kadhaa wanaendelea kusumbua wafanyabiasha kwa manufaa binafsi, kama unabisha nenda wzr ya kilimo kaulize
 


Naona mnabishana bure hapa,
Mmoja yupo kinadharia zaidi na mwingine kiuzoefu/kivitendo. Mwaka juzi/jana kulikuwa na tatizo kubwa la kuuza mazao nje ya nchi. Wanaokaa mipakani ndio wanajua nini kinafanyika,ni mpaka pale hali ilipokuwa mbaya sana ndio wakaruhusu kwa vibali, lakini mbona hawatoi vibali vya kulima?

Nchi hii ina sheria nyingi mno kwa jambo moja, je una tambua kuwa mkuu wa Wilaya anaweza kupiga marufuku mahindi yasichomwe mtaani kama biashara ktk eneo lake kwa gharama ya mkulima ambaye hakusaidiwa? Mfano, GOBO linalipa sana, lakini DC kapiga marufuku, mkulima atainukaje? Sasa hivi serikali imeshindwa kununua mahindi yote na kuhifadhi, lakini kama wakulima wakiwa na uhakika wa soko la Zambia/Kongo liko wazi hapana mtu angelalamika, lakini mvivu fulani sehemu A anasababisha mkulima mzuri sehemu B asiuze mazao yake, hapa ndio penye utata.
 
suala la madalali huniudhi sana. ila nafikiri ni nguvu ndogo sana inahitajika kuwatoa. mfano wakulima wa vitunguu wanashindwaje kuungana kumshinda dalali? ruaha mbuyuni kuna hata zaidi ya wakulima 30, wanashindwaje kuungana. wakulima wasipounganisha nguvu watanyonywa mpaka wabaki mifupa.
 
yaani inaumiza sana. leo nimekutana na mkulima wa viazi ananiambia mipaka ikiwa wazi gunia wanauza 30,000. mipaka ikifungwa ni 18,000 hadi 20,000. kwa maneno yake kasema kilimo cha viazi ni use**e. yupo anapiga kazi rungwe avocado co. huu ni unyonyaji mkubwa zana wa wakulima unaofanywa na serikali. pia bila kujua wanapoteza ajira na kudumaza kilimo.
 

Huyo jamaa amesahau kitu kimoja, hata hizo parachichi zamani zilikuwa sio issue mpaka suala la kusindika lilipoanza.
 
Huyo jamaa amesahau kitu kimoja, hata hizo parachichi zamani zilikuwa sio issue mpaka suala la kusindika lilipoanza.
unafikiri zake!? kaajiriwa na mzungu flani. angekuwa anaendelea na kulima viazi hiyo nafasi angemuachia mwingine na pengine na yeye angekuwa ameajiri.
 
unafikiri zake!? kaajiriwa na mzungu flani. angekuwa anaendelea na kulima viazi hiyo nafasi angemuachia mwingine na pengine na yeye angekuwa ameajiri.

Hapo pa kuajiriwa na Mzungu kufuga nyuki au kulima parachichi ndio napachukia sana, unakuta msomi wa SUA kaajiriwa na Mzungu afuge nyuki, wakati nyuki wapo hapa TZ, mbao za mizinga zipo hapa hapa, maua yapo,maji yapo na elimu anayo na soko lipo.

Tukirudi kwa huyo jamaa yako/na wengine, pale Tukuyu parachichi zipo miaka yote, ni mpaka alipokuja yule Mzungu na kuweka Kiwanda Kiwira ndio zimepanda thamani, hili ni tatizo la nchi nzima, mifano ni mingi, kwa leo tuzungumze na huyo wa parachichi. Mwambie ajifunze siri za kuotesha parachichi, kutunza, kuvuna na ku-park na hatimaye kusindika vizuri, ili na yy asiishie kuajiriwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…