Pendragon24
Member
- Aug 8, 2018
- 68
- 97
Ukitoa ubovu wa miundombinu iliyopo katika sekta ya usafirishaji na mapungufu yaliyopo kwenye makampuni ya usafirishaji tatizo kubwa lipo kwa mamlaka ya usafiri aridhini LATRA na serikali maana mapendekezo mengi ya abiria yamekuwa yakipuuzwa na wasafirishaji wamepewa kipaumbele.
Hali hiyo inawanyima haki wasafiri na mizigo yao hata mabadiliko ya kanuni, sera na miongozo haipo kwa ajili ya kumsaidia msafiri bali kuwaangamiza. Sekta ya usafirishaji ina changamoto nyingi ambazo abiria ndio mwathilika zaidi wa changamoto hizo.
Abiria anakutana na changamoto nyingi tangu siku ya kwanza ya kwenda kukata tiketi mpaka siku ya mwisho ya safari. Mabadiliko ya mara kwa mara ya ongezeko la gharama za usafiri na ukosefu wa ushirikishwaji wa wananchi ndio hasa vinaleta mashaka kwa abiria.
Abiria anakabiriwa na changamoto katika aina zote za usafiri kuanzia kwenye kusafirisha mizigo kwa njia ya mkokoteni,kusafiri yeye mwenyewe au mizigo yake kwa kutumia boda boda, taksii,huba,kilikuu, malori na zaidi kwa njia ya mabus.
Bond kubwa iliopo kati ya makampuni ya usafirishaji ndiyo inawaumiza abiria ambao wengi wao hawako organized hivyo kuifanya LATRA kupitisha mambo ambayo kwa asilimia kubwa ni upendeleo kwa wafanya biashara.
Changamoto hizo zimeshindwa kutatulika kwa muda mrefu, sasa zimekuwa sehemu ya maisha ya wasafiri ingawa wanaonewa ila hawana mahali pa kutoa kero zao hata wakitoa hakuna hatua inayochukuliwa dhidi ya wakosaji.
Abiria anakutana na mikiki wakati wa kukata tiketi kupandishiwa bei ya tiketi, siti moja kukatiwa zaidi ya abiria wawili na abiria kulazimishwa kusimama umbali mrefu akiaminishwa kwamba kuna watu watashuka mbele atapata siti.
Inakuaje wasafirishaji wa mabus wanaruhusu mtu kusafiri na watoto zaidi ya mmoja katika siti moja tena safari ya mbali na kusababisha kadhia kwa abiria wengine na saa nyingine kuhatarisha maisha ya watoto hao.
Inakuwaje abiria analipia nauli ya juu kwa ajili ya luxury bus lakini baada ya muda analetewa gari ambalo sio tu semi luxury bali ni bovu na haliendani na thamani ya nauli aliyolipia.
Katikati ya safari abiria wengi wanafaurishwa kwenda kwenye bus ambalo yeye halikuwa kusudi lake anafaurishwa kwenye gari ambalo ni la hovyo anapata usumbufu yeye na mizigo yake na kupoteza baaadhi ya mizigo wakati wa kufaurishwa.
Inakuwaje abiria akichewela bus kwa bahati mbaya au akishindwa kusafiri kwa ajili ya changamoto fulani asirudishiwe nauli yake kamili? kwanini sehemu ya nauli yake inakatwa ilihari ile siti yake imeuzwa kwa abiria mwingine huko njiani?
Wakati wa kupata chakula na kwenda kuchimba dawa mabus huenda sehemu ambazo wao wenyewe wanapata vyakula bure, huku abiria akinunua vyakula hivyo kwa gharama kubwa ambazo wasafiri wengi hawazimudu, hii inapelekea wengi kusafiri wakiwa na njaa hivyo kupelekea magonjwa ya tumbo.
Hata muda wanaotoa kwa ajili ya kupata huduma za chakula na kuchimba dawa ni mdogo sana unakuta watu wa siti za nyuma bado hawajashuka ila muda wa kurudi kwenye gari umefika na dereva anapiga honi tayari kuendelea na safari, hii inapelekea abiri wengi kuachwa na wengine kuchanganya magari.
Mabus mengi yanajaza abiria nje ya utaratibu wa siti zilizomo ndani ya bus, yapo mabus mengine ndoo zinafanywa kuwa siti ili kujaza abiria na mkifika sehemu ya mizani huoni hatua mahususi zikichukuliwa kwa uzito uliozidi kiwango cha kawaida cha bus.
Lakini pia huduma kwa wateja ndani ya bus kwa ujumla haziridhishi hata kidogo abiria anaweza kupata changamoto za kiafya njiani huoni msaada wowote kutoka kwa watoa huduma.
Bus linapata ajari na kusababisha ulemavu kwa watu na wengine kupoteza uhai lakini huoni mabus yakisaidia abiria hao kwa chochote wakati kampuni yao ndio imesababisha yote.
Askari wa barabarani waliotakiwa kusaidia haki za wasafiri wamekuwa wakiongoza uvunjwaji wa sheria za barabarani na ajari nyingi zimetokea kwa ajili ya uzembe wao.
Mtu anatuma mzigo wake kwenye bus inakuwaje bei ya mzigo inapanga kwa kukadiliwa kwa macho pasipo kipimo maalumu?
Haki ya kujua bei ya kusafirisha ule mzigo imo mikononi mwa kondakta ambaye ukimwambia nataka kutuma mzigo anakwambia ulete kwanza huo mzigo tuuone kisha ukiuleta anakutajia bei ya juu sana ambayo haina scale reference zaidi ya macho.
Imagine umebeba mzigo wako kutoka nyumbani mpaka stendi umetumia gharama za kuufikisha stendi ili tu kondakta wa bus aweze kuuona ili aweze kutaja bei,kondakta bila kuona mzigo hawezi kutaja bei ni lazima aone kwa macho yake kwanza.
Sasa kuelekea katika TANZANIA TUITAKAYO hizi ni baadhi tu ya njia zitakazo saidia kuleta uhalisia katika bei ya kusafirisha mizigo na kupunguza ghasia kwa wasafiri,

- Pawepo na kipimo maalumu (scale) kitakachoweza kupima (kama ilivyo posta) kwa haki na usawa ili kutambua bei halali ya kusafirisha mzigo, kama vipimo hivyo vipo basi viboreshwe na wahusika wasimamie ili viweze kutumika ipasavyo,hii itapunguza wasafiri wengi kuzidishiwa bei ambazo hazistahili.
- Kuanzishwa kwa chombo maalumu mfano wa mashirika yasiyo ya kiserikali mengi zaidi yatakayokuwa yanasimamia haki na usalama wa abiria na kutoa elimu kwa wasafiri ili waweze kutambua haki zao muda wote wa safari,mashirika yatasaidia kupambana na uonevu kwa wasafiri na mizigo yao lakini pia yatasaidia kuwaunganisha na kuwasemea abiria.
- Askari wa usalama barabarani asiruhusiwe kuwashusha abiria kwenye gari wakati wa kusafiri kwa kosa la dereva mamlaka itafute njia nyingine ya kumalizana na dereva kwani kitendo hiki kina wanyima haki kundi kubwa la watu wanao kwenda kwenye majukumu yao na kujenga chuki kati na askari.
- Sheria ya mamlaka ya uthibiti wa usafiri ardhini ya mwaka 2019 ibara ya 5 (1) (c)(iii) kiondolewe ili kuipunguzia LATRA majukumu ya kusimamia mabadiliko ya nauli badala yake waziri mwenye zamana apeleke swala hilo bungeni lijadiliwe, kwani swala la mabadiliko ya nauli lina waathiri wananchi wengi hivyo halipaswi kuamuriwa na taasisi kama LATRA pekee.
Mwisho, kilio kikubwa cha abiria ni swala la kupandishiwa nauli ambazo hazipo kwenye utaratibu wa kisheria sio tu kwa magari yanayokwenda mikoani hata madaladala na usafiri mwingine ndani ya mikoa abiria wengi wanapigwa na hakuna jitihada za maksudi za mamlaka kutoa elimu za mara kwa mara kwa abiria.
Upvote
5