Ili kuokoa soka la Tanzania Kasongo na Boimanda mjiuzulu

Ili kuokoa soka la Tanzania Kasongo na Boimanda mjiuzulu

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Hiki mlichofanya Leo ni aibu. Mkisoma barua yenu mnapata chochote cha maana Kwa nini mmeahirisha Mechi?

Mnasema Simba hawajulisha Mamlaka yoyote kwamba wanakwenda uwanjani muda Fulani kufanya mazoezi.

Nyie hao hao kwenye barua hiyo hiyo mnasema Simba walizuiwa na mabaunsa wanajulikana ni wa Yanga kuingia uwanjani. Kama Simba hawakujulisha kwamba wanakwenda uwanjani na Kwa mujibu wa barua yenu walipaswa kufanya hivyo huo Uhalali wa kuingia uwanjani unatoka wapi?

Mmegundua hao mabaunsa waliozuia Simba kuingia uwanjani ni wa Yanga na Kwa vyovyote walitumwa na Yanga Kwa nini mpange tarehe nyingine ya Mechi badala ya kuwapa Simba USHINDI maana waliovuruga Mechi Kwa maana hiyo ni Yanga?

Mmekuwa na madhaifu mengi kwenye uongozi wenu na hili la Leo limezidi. Jitafakarini tokeni muachie wengine.
 

Attachments

  • 20250308_142709.jpg
    20250308_142709.jpg
    174.3 KB · Views: 1
Na hii barua mmeandika nyie.
 

Attachments

  • 20250308_102105.jpg
    20250308_102105.jpg
    149.5 KB · Views: 1
Ni kwasababu Simba hatufurahii ushindi wa mezani.

Sisi kwetu point 3 tunazozihitaji ni zile ambazo tumezipambania uwanjani na sio sandakarawe.

Tunaopenda mpira tunataka kuipima timu kupitia ushindani, TFF wamezingua swala la kusema Simba haikufanya mawasiliano kwangu naiona kama haiko sawa.

Kwasababu kama kanuni zinasema katika muda fulani timu ngeni itafanya mazoezi, maana yake katika muda huo tajwa umiliki wa uwanja utakuwa chini ya timu ngeni.

Simba amefika ndani ya muda uliopangwa then anakutana na kizuizi tena dhidi ya timu pinzani huoni hiyo haijakaa vizuri?

Kwangu mimi hoja ya kusema Simba ilipaswa kufanya mawasiliano kabla ingekuwa na mashiko zaidi iwapo katika muda uliopangwa kwa timu ngeni kufanya mazoezi kusingekuwa na watu wenye vinasaba na timu ya Yanga badala yake wawe ni wasimamizi wa mechi na uwanja.
 
Back
Top Bottom