Ili kuondokana na tozo, Serikali ihalalishe gongo, kilimo cha bangi na kurasimisha pombe za kienyeji

Ili kuondokana na tozo, Serikali ihalalishe gongo, kilimo cha bangi na kurasimisha pombe za kienyeji

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Ili kuongeza wigo wa mapato yatupasa kama taifa kuthamini na kuzalisha vya kwetu. Tusiwe mabingwa wa kukopi na kupesti tu.

Mfano Usafiri wa bodaboda ulianzishwa miaka mingi nchini Nigeria kabla yetu. Kwa Afrika mashariki nchi ya kwanza kuruhusu bodaboda kuwa chombo cha kubeba abiria ni Uganda. Na hata jina bodaboda kimetokea huko. Ndipo baada ya kuhelewa sana tukafanya maamuzi ya kukopi na kupesti.

Gongo na pombe nyingine za kienyeji zinatumiwa Sana nchi nzima. Kwann serikali kupitia TMDA/TFDA, TBS na mamlaka nyingine zisiwasaidie watengenezaji wa vileo hivi namna bora ya utengenezaji na packaging ili viwe vinywaji vyenye ubora wa kitamataifa? Kisha tuuze ndani na nje ya nchi?

Lkn pia turuhusu kilimo cha bangi (sijasema turuhusu matumizi) kama inavyofanyika Afrika ya Kusini, Rwanda na nchi nyingine za Ulaya na baadhi ya majimbo ya Marekani. Zao hili linaweza kutuingizia fedha nyingi za kigeni.

Tuache ushamba wa kukamuana kwenye tozo tuuu huku tukiendelea na uvivu wa kufikiria nje ya boksi.

Pia waweza kisoma:-

 
Kwanini Serikali isibane kwenye madini?
Unajua madhara ya unywaji wa Gongo?
 
Madada poa nao warasimishwe wawe wanalipa kodi ili kuleta nafuu ya mzigo wa tozo.
 
Pia wachungaji na mashekh ubwabwa walipe Kodi expect wasuni tu
 
Umesomeka vizuri hata Wajackoyah kule Kenya alilitaka Hilo kwani linakuza uchumi.
 
Unajua madhara ya unywaji wa Gongo?
Ninyi watoto hamjawahi kunywa Gongo, tuulizeni sisi, Gongo madhara yake ni kama Gin zingine zinazouzwa kaunta.

Tena likitengenezwa huku wametulia bila kuogopa polisi, Gongo linaiva na ni lenye kuburudisha.
 
Ninyi watoto hamjawahi kunywa Gongo, tuulizeni sisi, Gongo madhara yake ni kama Gin zingine zinazouzwa kaunta.

Tena likitengenezwa huku wametulia bila kuogopa polisi, Gongo linaiva na ni lenye kuburudisha.
Mwambie huyo dogo. 90% ya mawaziri, wabunge na madiwani wamesomeshwa na gongo. Gongo inanywewa na 70% ya watanzwnia.
 
Back
Top Bottom