Ili kuua mvutano wa serikali mbili au tatu, basi iwepo serikali moja ya Tanzania

Ili kuua mvutano wa serikali mbili au tatu, basi iwepo serikali moja ya Tanzania

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Mie naona ili kumaliza mgawanyiko na mvutano unaojitokeza kuhusu Tanzania kuwa na serikali mbili au tatu, basi tuwe na serikali moja. Maana kama suala ni kuua kero za muungano na kuuimarisha, basi serikali moja ndio jibu la yote.

Serikali moja Tanzania ni jambo linalowezekana, kama kweli tuna nia ya kuimarisha muungano na hatuongei unafiki.
 
Watu wameshaanza kudai nchi yao ya "PEMBA" wewe unaleta habari y serikali moja?...
 
Ama serikali moja,au serikali tatu kama sivyo muungano UFE!
 
Ukimuuliza Rais wangu mpendwa Dr Kikwete , Je unapenda Muungano jibu lake litakuwa kweli ninaupenda na nitaulinda kwa nguvu zote
Ukimuuliza Dr Sheni naye majibu yatakuwa yale yale,
Ukiumuuliza Nape na maccm wote wa bara na Zanzibar woooote jibu ni lile lile wanaupenda wnaulinda na kuuenzi.
SASA waulize swali lingine , KAMA mnaupenda na mnaapa kuulinda kwa NGUVU zote hizo basi TUUNGANE kisawasawa Tanazania iwe SERIKALI MOJA !!!!!!!!!!!
Du hapo ndo utaona unafiki wa wanasiasa, kila mmoja ataondoka amenyongonye hatakupa JIBU
WANASIASA MNATUCHANGANYA AKILI SABABU YA UROHO WENU KUNA MNACHOFAIDI AMBACHO HAMTAKI KUKIWEKA WAZI !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mtoa mada,suluhisho kila mtu afe na chake.
 
ah,,,ww hujui ata hii tanzania inatoka na nn!,,,serikali moja haiwezekan ata iweje mwana,,husikurupuke tu,,,hebu fuatilia kwanza,,
 
Ikiwa serekali moja yaani ya Tanzania pekee, basi ina maanisha hapo mwanzo hakuwa na muungano, maana Haiwezikani mahakama ikatoa hukumu ya hisa zote kupelekwa mrengo mmoja tu ikiwa company hiyo ilikuwa imeundwa na watu wenye hisa tofauti. Haiwezikani uvunje muungano wa nchi mbili na kuzua tu serikali moja, kwanza italazimika kuigawa sehemu mbili ndipo yatoke maamuzi je ziwepo serekali mbili. Mi nahisi hii rasimu isinge tungwa kabla. Nadhani ingelikuwa vizuri muungano kuvunjika kwanza halafu tukajitia kujishughulisha ni chaguo gani la busara, kuwa ni SEREKALI MOJA, SEREKALI MBILI AU SERIKALI TATU. Hapo ndipo tutaweza kujua nani anahamu na muungano na nani anaathirika na muungano na nani anafaidika. Kila mmoja angelitoa mawazo ya ndani ya mtima juu ya alivyokuwa akiupenda muungano au kuuchukia. Langu mimi ni hili
 
Back
Top Bottom