Ili kuuonyoosha Uongozi wana Simba SC tungekuwa na Akili tungesusia kwenda Viwanjani, ila kwakuwa tunapenda Kudanganywa kama Kuku tunaenda tu

Nikiambiwa kwa sasa nitoe Alama za Kikosi cha Simba SC cha sasa baada ya Kukiona natoa ni 10% tu, ila 90% Kibovu.
Mtanzania hana umoja linapokuja suala la maslahi muhimu. Si mpira tu hata nchi yake, ila kwenye mambo ya hovyo utawaona
 
Mbinu na matendo ya siasa yabaki hukohuko kwenye siasa. Soka huwa halitaki hayo mambo ya kususa susa. Huwa tunatoa tu maoni na kutoa muda kwa timu kuyafanyia kazi. Basi.

Ova
 
Ligi ikianza watu watatukanana na kununiana msimu mzima,. Msimu ukishaisha MO atatangaza tena kuwa “sasa narudi Simba”, mashabiki nao wataipokea na kuanza kumuimba “Bosi Karudi” kuongoza Simba raha😅, just wela watu wakuwa wanaanzisha nyimbo uzitakazo tu
 
Shida ni kwamba, ukiona Simba inacheza unaona timu haina tatizo iko vizuri tu, ni matatizo madogo madogo.

Daah,

Ukija kuiona Yanga unaona kabisa Simba wanacheza ujinga na hawako serious🤣🤣🤣
Aaahaaa

Kwahiyo ni Bora Yanga wasicheze basi
 
Tunaambiwa striker mpya ana mashuti hatari.

Akipiga mpira unaenda mpk mwezini ungonga mwezi, halafu mwezi unagonga jua na kusababisha solar eclipse.

Maneno ya uwongo wa wazi kabisa haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…