Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Salaam wakuu,
Moja wapo ya Initiatives za awamu ya tano katika kuboresha maisha ya watu wake ilikuwa ni kuwatambua na kuwaruhusu wafanyabiashara wadogo qadogo, jambo hilo lilifanikiwa kwa asilimia kubwa na kuiwezesha serikali kupata mapato yake.
Awamu ya sita (6) imeonekana kutokuwa mbali sana na awamu ya tano hivyo sitegemei kuona mabadiliko makubwa katika hili.
Baada ya kuwatambua wafanyabiashara hao ili kuwawezesha kukuza mitaji na kuboresha maisha yao kwa kuweza kuipata mitaji hiyo toka taasisi mbali mbali za kifedha ni vyema sasa serikali ikaona umuhimu wa kuviboresha vitambulisho vya machinga, kwa kufanya hivyo si tu kutawasaidia machinga bali kutaifanya serikali kupanua wigo wa kodi kuliko kutegemea vyanzo vile vile vya mapato.
Kupitia brela upo utaratibu wa mtu mmoja kurasimisha biashara yake kwa kusajili jina la Biashara, (business name) utaratibu ambao utamuwezesha mhusika kuwa na namba ya mlipa kodi ama TIN.
Kumuondoa machinga kutoka kumiliki kitambulisho pekee mpaka kumiliki jina la biashara itakua hatua kubwa ya kumfanya kuwa mmoja wapo wa washiriki katika kukuza uchumi kupitia kodi na kumfanya kuongeza kipato chake kwani itakuwa rahisi kwake kuaminika na si tu taasisi za fedha ambazo anaweza pata mikopo bali na watu binafsi na jamii kwa ujumla.
Naamini kwa dhamira hii ya serikali ya kuboresha maisha ya watu itazingatia na kuufanyia kazi ushauri huu.
Wasalaam,
Statesman.