SoC03 Ili tuendelee, tunachotakiwa kubadili ni mindset ya watu wetu kwanza

SoC03 Ili tuendelee, tunachotakiwa kubadili ni mindset ya watu wetu kwanza

Stories of Change - 2023 Competition

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Wahenga wanasema kuishi kwingi ni kuona mengi. Hakika, katika safari yangu hapa duniani, nimekua najiuliza maswali mengi sana ili kupata utambuzi wa identity yetu sisi watu weusi na kwanini tuko katika hali hizi zetu duni.

Mara nyingi, lawama zinatupwa kwa wakoloni, yaani wakoloni weupe (wazungu na waarabu) waliokuja kututawala physically. Kwamba, hao ndiyo wameiba rasilimali zetu nyingi na kutuletea elimu mbaya isiyokidhi uhalisia na matarajio ya vizazi vyetu.

Hali kadhalika, lawama zinatupwa kwa wakoloni wapya, hawa ni viongozi waliopigania uhuru wakawa ni wakoloni wapya, ambao walipora fedha za umma na kujilimbikizia mali na kutuacha kwenye dimbwi la madeni na umasikini wa akili na kipato.

Aidha, kuna falsafa nyingi sana kwenye mapambano dhidi ya umasikini na ufukara wa mtu mweusi. Wapo wanaosema na kudhani ili tuendelee tunahitaji ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora. Lakini wapo wanao amini kwamba uwekezaji ufanyike kwenye elimu haswa ya ugunduzi itakayo leta ushindani kwenye soko la dunia na kutuweka kwenye nafasi shindani katika ramani ya dunia.

Lakini ninajitafakarisha na kuona kwamba, ili tuendelee tunahitaji mabadiliko ya fikra (change of mindset).Sisi watu weusi tunapaswa kujua kwamba hatuishi kwaajili yetu bali kwa ajili ya vizazi vijavyo. Jamii zote za kitanzania zinapaswa kujiendesha huku zikizingatia hilo.

Kama tukiishi kwa nidhamu ya kujua uwepo wetu ni maandalizi kwa ajili ya vizazi vijavyo, sehemu kubwa ya matatizo yetu itakua imetatuliwa.

Kwa nidhamu hiii, hapatakuwepo mtu atakaye fanya mambo yafuatayo:

1. Hakuna mtu atakaye uza rasilimali zetu kwa wageni ( ile hadithi ya chief mangungo wa msyovelwa ingekoma baada ya kifo cha huyo infamous tribal leader);

2. Hakuna kiongozi angefanya ubadhirifu kwenye mali za umma ili hali akijua wajukuu zake ndiyo wanufaika wakubwa,

3. Hakuna mtu angechafua mazingira yaani atakaye kata miti hovyo na iana zote za uchafuzi wa mazingira, kwa maana mazingira yetu ni urithi wa vizazi vya sasa na vijavyo;

4. Hakuna mtu kwa maana ya wawakilishi wetu wangekubali kupitisha sheria kandamizi na onevu ili hali akijua watoto na wajukuu zake watakutana na mkono mkali wa hizo sheria; na

5. Na hakuna mdau yoyote wa elimu angekubali elimu mbaya isiyo lenga kufundisha vijana kuyamudu mazingira yao iendelee kutolewa

Kwa muktadha huo, wale wenye mamlaka wanapaswa kuchochea hii mentality kwa watoto wetu. Watoto wafundishwe mapema kabisa, kuanzia shule ya chekechea elimu ya uzalendo, kuipenda nchi yao na kufanya yale mema ambayo yatakua ni urithi kwa vizazi vijavyo.

Taifa liwe na tabia ya kuwaenzi wale waliofanya mema kwa nchi yao kwa uwazi bila ya kuingiza siasa. Pia liwe na utaratibu wa ku-shame wale walio fanya vibaya bila ya aibu.

Hitimisho, ni wasiwasi kwamba wajukuu zetu watasema nini kuhusu sisi, je hatuta kua ni muendelezo wa hadithi ya chief mangungo na genge lake.

Ni imani yangu, kila mtu kwa nafasi yake anao wajibu na jukumu la kuboresha. Tujenge taifa lenye heshima ili tuweze kujiheshimisha kwa wale watakao soma historia zetu.

Nawasilisha.
 
Upvote 7
Wasilisho hili linafaa kuwa muongozo kwa wanaoaminiwa kushika madaraka kwenye ngazi zote za Idara na Wizara na zaidi sana mihimili yote mitatu ya nchi yetu. 🙏
 
Wasilisho hili linafaa kuwa muongozo kwa wanaoaminiwa kushika madaraka kwenye ngazi zote za Idara na Wizara na zaidi sana mhimili yote mitatu ya nchi yetu. 🙏
Hakika
 
Back
Top Bottom