Ili tuharakishe maendeleo, Miji mikubwa na mabasi ya mikoani vifanye kazi 24/7

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Hakuna haja ya kufunga, kuzima taa na kuegesha mabasi wakati tunashughuli ya kukimbiza UCHUMI wa TANZANIA.

Kwanini miji kama DAR ES SALAAM, MBEYA, MWANZA, ARUSHA, KAHAMA, MAFINGA, TUNDUMA BORDER nk ifungwe? Nyakati za usiku?

Kwanini mabasi yasisafiri usiku!? Je, hatuwezi kuimarisha ULINZI highway na kwenye Town centers zilizobainishwa ili tukuze uchumi hasa maeneo yenye moto wa biashara kama baadhi nilotaja hapo?

Naomba SERIKALI mlifikirie hili suala. Ndugu WABUNGE kwa umoja wenu iagizeni serikali ilitafakari suala hili.

Wenzetu wanatuacha baadhi ya town centers ziko active muda wote...pia abiria wanasafiri usiku/mchana.

TUBADILIKE kama kweli tunanuia kukuza uchumi kwa haraka kwenye ukanda huu. TUNAPOTEZA rasilimali nyingi kwa kulaza MIJI YETU na USAFIRI. Hayo ni mabilioni yanakuwa USINGIZINI.

Jeshi letu la POLISI liongezewe rasilimali WATU na rasilimali VIFAA ili tutekeleze hili. Biashara pekee inaweza kutuinua pakubwa sanaaa...Cross border business itakua kwa kasi.

Kwa kuanza mkakati huu tufikirie kufunga Street Cameras na lights....kisha Jeshi letu lipewe vifaa na watu wa kutosha...kisha tuchague miji kadhaa ambayo itakuwa SLEEPLESS CITIES kv Mwanza, Mbeya, Dodoma, Dar, Tunduma, Mafinga,Kahama to mention but a few.
 
Ili kuharakisha uchumi wetu huo kupitia bara bara naombeni mtuondolee vibao vya 50 na tochi za barabarani! Waweke kibao cha 80KPH sehemu za kunyunyuzia!

Madaraja ya juu yawekwe kuvusha wapita kwa miguu!
 
Wazo la msingi nadhani tukipata highway za uhakika kama ile ya Mafinga-Igawa au Kimara Kibaha Highway 80KPH inawezekana kabisa magari hata 8 yanapishana.

Lakini wazo hili lije na kupiga marufuku MAGARI makuukuu yenye umri unaozidi miaka 7. Tuwe na vitu vya uhakika 10yrs iwe kwa magari ya mizigo....private ziwe ni miaka 7 zaidi ya hapo mtu apigwe kodi x5 yake
 
Ili kuharakisha uchumi wetu huo kupitia bara bara naombeni mtuondolee vibao vya 50 na tochi za barabarani! Waweke kibao cha 80KPH sehemu za kunyunyuzia!

Madaraja ya juu yawekwe kuvusha wapita kwa miguu!
Hakuna kitu kina kera wageni nchini mwetu kama 50kph na matuta yaliyopo bara bara kuu zetu, mahala pakutumia masaa 2 sisi tuna tumia 4 mpaka 5. ukitaka kuamini angalia usafiri wa basi toka Dar-Sumbawanga. Dar-Bukoba. Dar-Musoma , kuna saa madereva wanaendesha kama wehu wanaruka matuta bila hata kujali usalama wa abairia kikbwa wafanikiwe kufidia muda.
 
Matuta ni mengi halafu hayana maana! Sehemu zenye Zebra highway wawekege madaraja ya juu tu
 
Hata madaraja ya chini ya ardhi kama pale Iringa na hali inakuwa shwari kabisa, matuta ya pale ubungo yameshaanza kutoa maana ya daraja na njia mpya
 
Wameongeza matuta tena?
Ukitoke upande wa juu wameweka pale karibu na tenk la maji ukitokea upande wa mjini wameweka pale karibu ya kuingia Tanesco, last week walikuwa sijui wanayaongeza ukali maana yamekuwa sharp zadi, kuna madereva wana kuja toka south wanalalamika sana juu ya 50 na matuta nakukamatwa kwenye Zebra za kwenye bara bara kuu, kwakweli wataalamu wetu sijui ni usingizi gani wamelala.
 
Pale zebra za Tanesco palitakiwa pawe na daraja kama la buguruni la kupita juu ili kusiwe na disturbance kwa chini pale!
 
Mkuu haya ya juu yana Challenge kwa sisi watu wa Logistics hata lile la buguruni huwa linatusumbuwa pindi tunapo pakia mizigo mirefu amabayo haiwezi kupunguzwa huwa ni lazima tungojee usiku na vibali ndi mzigo utoke port, kwakweli wataalamu wetu huwa hawaangaliagi kila upande wao huwa wanaamua wanavyotaka wao tu na wakijua hatuwezi kuwahoji, TATOA ilishawahi piga kelele lakini majibu yake yalitoka hapo utazania wao sio wawekezaji ktk Nchi hii.
 
Kwahio mnashauri daraja liwe under ground
 
Lawaenda kwa miguu sawa kabisa kama la pale Iringa Njia ya kwenda juu inapunguza sana msongamano kwakweli. Au hii njia sita ya kibamba ni kisu aisee inakata kila siku, sasa ukiweka la juu kwakweli 5.5 huwa inatusumbuwa sana hata lile la Ruvu 5.5mt lakini kuna kipindi tunapita nnje ya njia kuu na nikwa gharama zetu.
 
Tujenge taifa kwa saa 24.shughuli za kiuchumi ziendelee saa 24.
Nchi za Wenzetu wanatuacha,sisi tunalala.

Wenzetu shughuli za kiuchumi zinafanyika saa 24,sisi tunajipa uoga tunasema hakuna kusafiri usiku.
Tuache yoga tuzungushe uchumi,mzunguko wa fedha uongezeke, uchumi ukimbie kwa kasi:
Wenye mabasi,wanaweza kuongeza biashara mara 2,kuwa na mabasi ya mchana na usiku.
Wenye viwanda wanaweza kuwa na uzalishaji mara 2.usiku na mchana.
Wauza chakula watauza mara 2,usiku na mchana.
Uchumi utakuwa usiku na mchana kama nchi zinazotuzidi kiuchumi, wao shughuli za kiuchumi zinakimbia sio kutembea.
Ajira zitakuwa mara 2,wale wanaofanya kazi mchana,na wengine usiku.
Kipato kitaongezeka mara 2,fedha itaingia mchana na usiku.
Treni ifanye kazi usiku na mchana,abiria wasafiri mchana na usiku(huu ni usafiri usio kuwa na mpinzani,shirika litapata fedha mara 2 zaidi).
ANGALIZO:Serikali,mfunge kamera maeneo yote muhimu.
 
Ili kuharakisha uchumi wetu huo kupitia bara bara naombeni mtuondolee vibao vya 50 na tochi za barabarani! Waweke kibao cha 80KPH sehemu za kunyunyuzia!

Madaraja ya juu yawekwe kuvusha wapita kwa miguu!
Hili la speed mwanabodi inabidi mabarabara yatanuliwe kwanza. Kwa sasa mabarabara yetu Mengi ya highway bado ni membamba
 
Tujenge taifa kwa saa 24.shughuli za kiuchumi ziendelee saa 24.
Nchi za Wenzetu wanatuacha,sisi tunalala.

Wenzetu shughuli za kiuchumi zinafanyika saa 24,sisi tunajipa uoga tunasema hakuna kusafiri usiku.
Tuache yoga tuzungushe uchumi,mzunguko wa fedha uongezeke, uchumi ukimbie kwa kasi:
Wenye mabasi,wanaweza kuongeza biashara mara 2,kuwa na mabasi ya mchana na usiku.
Wenye viwanda wanaweza kuwa na uzalishaji mara 2.usiku na mchana.
Wauza chakula watauza mara 2,usiku na mchana.
Uchumi utakuwa usiku na mchana kama nchi zinazotuzidi kiuchumi, wao shughuli za kiuchumi zinakimbia sio kutembea.
Ajira zitakuwa mara 2,wale wanaofanya kazi mchana,na wengine usiku.
Kipato kitaongezeka mara 2,fedha itaingia mchana na usiku.
Treni ifanye kazi usiku na mchana,abiria wasafiri mchana na usiku(huu ni usafiri usio kuwa na mpinzani,shirika litapata fedha mara 2 zaidi).
ANGALIZO:Serikali,mfunge kamera maeneo yote muhimu.
Kabisa aisee
 
Ingawa sio rasmi lakini Kuna magari yanasafiri usiku. Kuna siku nimetoka Dodoma saa Moja na kuingia Iringa saa SITA usiku. Kwenye bus kulikua na abiria wengi wa Mbeya ngoma iliunga probably Mbeya wakiingia asubuhi. So ikiwa rasmi suala hili linawezekana.
 
Kama mabasi yanaruhusiwa kutembea usiku sawa, japo sina Uhakika kamą ni rasmi, wadau watakuja watueleze
 
Back
Top Bottom