Ili Ufanikiwe-Lazima Ujitoe Ufahamu

Ili Ufanikiwe-Lazima Ujitoe Ufahamu

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Umewahi kujitoa ufahamu?Umewahi kuona mtu ambaye amejitoa ufahamu?Unaelewa ufahamu ni nini?Una ufahamu?

Nitaanzia Mwishoni.
Miaka zaidi ya 15 iliyopita nilianzisha kampuni yangu ya kwanza,Nikafungua akaunti na kupata cheque book nikawa ni mmiliki wa Kampuni.Pesa nilizotumia kufanya hivyo zilikuwa ni za ada ya Chuo.Strategy yangu ilikuwa simple tu.Niwe na kampuni nipige Pesa.Kwenye kampuni yangu mimi nilikuwa tarishi aka messenger na mimi nilikuwa mkurugenzi mtendaji aka MD.Nikitazama nyuma sasa najua kwamba nilijitoa ufahamu.

Ndani ya kipindi kifupi cha miaka mitatu niliweza kutengenza Revenua ya zaidi ya Milion 30 na kuwa na wateja zaidi ya 200 katika biashara yangu.

Wateja wangu wengi walikuwa wanajua mimi ni mtumishi tu ni kwamba Mkurugenzi alikuwa BUSY mara yuko Japan,China,UK. na mimi ndo mwakilishi wake.Jina la mkurugenzi lilikuwa jina la Mpenzi wangu ambaye hata hakuwa anajua kuwa katika rekodi ya jamhuri alikuwa Mkurugenzi wa kampuni.Alikuwa ni mwanafunzi tu..
\Nilifanya kazi na kampuni kubwa za ndani na nje ya nchi na nilikuwa naenda kwenye meeting za kibiashara nikiambatana na warembo ambao kazi yao ilikuwa ni kuchukua notes za meeting to na kutabasamu na kutingisha kichwa.Nilikuwa na umri mdogo tu ila nilikuwa nimejitoa ufahamu.

Ufahamu ni nini?Ufahamu ni ile hali ya kuwa na uwezo wa ung'amuzi na uelewa unaokufanya ama upate ujasiri wa kuamua au kufanya jambo au ukose ujasiri wa kuamua au kufanya jambo.Unapojiyoa ufahamu unaamua kuangalia upande mmoja tu wa sarafu yaani ule unaokuvutia na wenye faida na kuamua kuutumia kufanya maamuzi.

Il ufanikiwa kwa urahisi kuna wakati inabidi ujitoe ufahamu kwa kiwango cha Juu..

Je umewahi kujitoa ufahamu?Tujadili hapa faida na hasara za kujitoa ufahamu mintarafu mafanikio.

Wasiliana nasi kwa njia ya email.masokotz@yahoo.com ili upate taarifa za mafunzo yetu ya Fursa na usimamizi wa Biashara.

Kumbuka NO SALES no BUSINESS.Kama biashara yako haina mauzo basi hauna biashara

Karibu tujadili
 
Kampuni umeanza kutengeneza pesa...bado upo kwenye mfumo email za buree...hiyo pesa unayoitengeneza hujui kazi yake...ivi yahoo.com kweli ni email ya watu wenye mtandao mkubwa kama ulivyotuhabarisha....? badilika bwana ata kama umeamua kujitoa ufahamu jaribu japo kidogo kupunguza speed
 
kampuni umeanza kutengeneza pesa...bado upo kwenye mfumo email za buree...hiyo pesa unayoitengeneza hujui kazi yake...ivi yahoo.com kweli ni email ya watu wenye mtandao mkubwa kama ulivyotuhabarisha....? badilika bwana ata kama umeamua kujitoa ufahamu jaribu japo kidogo kupunguza speed
Mkuu, kwani kutembea na miguu kuna maana mtu hana gari? Anyway nimepokea ushauri wako nimeufanyia kazi.
 
Naona unaendelea kujitoa ufahamu, ngoja waje utawapata tu!
 
Kwahiyo umejitoa ufahamu ukaamua uje ututoe na sisi?
 
Back
Top Bottom