Ili ufanikiwe maishani kipi kitangulie gari, nyumba au ndoa?

Kwangu gari kwanza, nyumba ntajenga ile nnayotaka mimi pale ninapotaka.
 
Ndoa kwanza sababu hiyo hata gharama zake ukiamua zinaweza zikawa zero,lakini nyumba na gari unaweza kuwa nazo nyingi tu kiasi cha kukusumbua kuhesabu au unaweza kuzeeka haujawahi kumiliki japo kiwanja wala driver's license.
 
anza na biashara hata kama ni ndogo ndogo kasha jitahidi uwe na usafiri kurahisisha safari za kufuata mali na kufuata wateja kasha oa (ndoa) kasha nyumba (Usisahau kujiendeleza kielimu)
 
na usijenge kwa kutumia mshahara utatumia miezi 50

pia kama anategemea mkopo au mshahara bila biashara itamsumbua na itamchukua muda
Jamani, kuna mishahara mingine, tena ya watu wengi tu, ni mikubwa kuliko biashara nyingi sana. Tunaposema usitegemee mshahara fanya biashara, mshahara wake tunaujua?
 
Du swali zuri unaweza ukaanza kuoa na ukapata mke bora yote yakafwata unaweza kujenga ukaja ukaoa mke wa matanuzi vyote vikapotea muhimu muombe mungu awe ndio muongozi wako yeye Allah ni mjuzi wa yote binadamu tunajaribu tu
 

Anza na gari, na kama tayari umeshajenga nyumba, uza nyumba ununue gari!
 
Kujitafakari ni muhimu zaidi kwani inakupasa kutambua umri ulionao.
malengo na nia.
hofu umefika miaka 45 huna vyote.
 
hakuna formula katika kufanikiwa kimaisha!ni vile tu wewe unavyojipanga ukitumia fursa zilizopo kwa juhudi na maarifa!
 
Maisha hayana formula. kwan maisha ni nyumba na gari pekeyake!?
 
Nyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…