Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Natoa ushauri huu kwa serikali, sitarudia tena maana Mimi nina kazi yangu na nina biashara zangu.
Umaskini na ufukara bado ungalipo hapa nchini.
Serikali sasa haina budi kujenga chuo Cha fundi kila kata au Kijiji na kupeleka walimu na vitendea kazi.
Vijana wasome bure, yaani kila kijana aliye tayari serikali igharamie masomo yake mpaka ngazi ya cheti cha awali, na watakaofaulu vizuri wasomeshwe mpaka ngazi ya stashahada (Diploma).
Kwa watakaotaka kuendelea na ujuzi ila hawana pass za juu wachangie asilimia kidogo na serikali iweke kilichobaki.
Hapo tutaona Mapinduzi ya viwanda kwa vitendo.
Vijana watafanya mambo ya ajabu na makubwa.
Gharama ya ndege 5 za abiria inaweza kufanya hili jambo kwa ushindi mkubwa.
Wananchi wataiheshimu serikali, wapinzani tutaiheshimu serikali.
Umaskini na ufukara vitaondoka kirahisi kabisa.
Msitujazie ma flyover huku vijana wengi hawana ujuzi wapo tu mitaani.
Hawa wamachinga hawakuzi uchumi wa Tanzania kwa asilimia kubwa bali wanakuza uchumi wa Uchina ambako bidhaa zinatoka
Hizi kozi zingine kama Human resources, Accounts, Social works and alike sasa zianze kupunguzwa na NACTE na TCU wakati wa udahili na usajili wa vyuo vipya.
Pia serikali iwe inaweka ligi ya kiufundi miongoni mwa vijana na washindi 100 au kumi kupewa zawadi kila mwaka. Zawadi hizo ziwe mitaji/fedha au vitendea kazi.