Ili ufukara uwaondoke Watanzania Serikali ifanye jambo hili

Mawazo mazuri tu,tatizo tz hatuna vision ya miaka mia mbele KILA ajae Kama kiongozi huja na vision zake, hushauri wako hauwezi kuja tekelezwa mkuu
 
Hilo lilikua ni lengo la Magufuli kujenga VETA kila kata kingine Waziri mkuu kila mwaka anatoa nafasi za bure kwa vijana wenye fani ambao hawana vyeti na kufundishwa kwa muda wa miezi 6
 
KWA KATIBA ILIYOPO hata Nchi iwe na MIAKA 120 ya UHURU UMASIKINI na UFUKARA hautaondoka NCHI ina LAANA

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Hilo lilikua ni lengo la Magufuli kujenga VETA kila kata kingine Waziri mkuu kila mwaka anatoa nafasi za bure kwa vijana wenye fani ambao hawana vyeti na kufundishwa kwa muda wa miezi 6
Elimu ya veta ndio ukombozi pekee wa masikini na kumaliza tatizo la ajira nchini.
Elimu ya chuo kikuu inaongeza idadi ya masikini nchini
 
Ahsante Ndugu, andiko linafikirisha kweli kweli aisee.
 
Afu kila mtu akiwa fundi ndio maendeleo yatakuja? πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† .

Ndugu acha wachumi watunge sera za maendeleo..Unapozungumzia maendeleo ni forward and backward linkages among multisectors..

Hakuna sekta moja inaleta maendeleo zote zinategemea a..

Japo kwa Maoni yangu vitu vya muhimu kabisa ni elimu yenye tija, miundombinu ya uchumi kwa upana wake na purchasing power( Kodi na sera za kuongeza kipato kwa mtu mmja mmja?
 
Na hivyo vyuo vya veta vijikite kwenye teknolojia za kusindika mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, madini na rasilimali nyingine zinazozunguka maeneo yao, na pia teknolojia kwa ajili ya makazi bora ya watu, huduma za kijamii mfano, vipuri vya magari, bajaji, bodaboda, mawasiliano, nguvu za kuzalisha umeme, miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji na ufugaji samaki.
 
Ni sawa hivyo vyuo vya veta vitajengwa, lakini vinahitaji ubunifu na akili kubwa inayoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, maoni yangu inatakiwa tuwekeze kwenye akili za watu kwanza.

Akili za watu zikikaa vizuri, basi watu wataenda mbali zaidi na kubuni na kutengeneza mashine na vifaa mbalimbali kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini. siyo mtu mweupe aunde kitu halafu sisi tuwe ndo wakurekebisha vitu hivyo kwa taaruma za kutoka Veta.

Watu wabunifu wapewe motisha, ikiwezekana kijana aliyebuni kitu fulani amazing, then direct anapata ajira na kuendelea kubuni zaidi, hii itasaidia watu kutumia misuli ya kichwani vizuri siyo kulala lala tu na kuwaza ngono tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…