Babu Kijana
JF-Expert Member
- Jan 24, 2013
- 587
- 276
Naungana na wewe 100%. Kimsingi hakuna nafasi ya kuipata pepo bila kwanza kupitia kifo.Hili ni wazo langu kwa Taifa stars, mabingwa wote huwa mabingwa kwa kuwafunga mabingwa, msitegemee timu za ki-chadi chadi, sasa imejitoa na group limebaki na Nigeria na Egypt na Tz, point zimepunguzwa kwa kila timu ilomfunga chadi. Tukomae tuwafunge hao waliobaki
Na je Chad isingejitoa tungeweza?Kimsingi hakuna cha muhimu kilichobadilika kwa Chad kujitoa.Cha tofauti ni kuwa tungemaliza nafasi ya tatu kwenye group ketu kama wasingejitoa.Wao wangekuwa wa mwisho.Nafasi ambayo haitupi chochote.Baada ya kujitoa tutamaliza nafasi ileile ya tatu lakini wa mwisho.Sasa kama tunamlalamikia Chad kujitoa basi tunamlalamikia kwakuwa amesababisha tuwe wa mwisho kwenye group.A thing which is ridiculous!Shida ni je tutaweza?