Ili uweze kufanikiwa unahitaji

Ili uweze kufanikiwa unahitaji

Ibun Mallik

Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
41
Reaction score
11
Mafanikio ni maendeleo ya kutoka hatua Moja ya maisha kwenda hatua nyingine, mafanikio hayo yanaweza kuwa katika nyanja mbalimbili ikiweno kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Watu wengi sana Tanzania na Duniani kwa ujumla wamekuwa wakiwaza na kutafakari kwa namba gani unaweza kufanikiwa kiuchumi. Sasa muarubaini wa hili umepatika.

Njia au namna mbalimbali za kufanikiwa kiuchumi.

KUJUA VIPI UTAPATA FURSA/NAFASI

Ili uweze kufanikiwa lazima kwanza ujue wapi na kwa vipi utapata nafasi ya kuekeza au kufanya biashara, vijana wengi hushindwa namna ya kupata fursa kwa ajili ya kuanzisha biashara. Zipo njia mbalimbali za kupata fursa ikiwemo kugundua tatizo na kutafuta suluhisho lake, kusoma katika vyanzo mbalimbali vya habari, kutumia uwezo ulionao katika kufikilia na kujifunza kwa kutembea sehemu zengine.

KUJUA NAMNA YA KUPATA MTAJI

Mara baada ya kupata nafasi jambo lengine ili ufanikiwe lazima ujue namna ya kupata mtaji kwa ajili ya kuanzisha shughuli furani ya kiuchumi. Pia hili ni tatizo kwa vijana wengi kujua wapi anapata mtaji, Kuna njia mbalimbali ikiwemo kukopa kwenye taasisi za kifedha, kutunza mwenyewe pesa kidogo kidogo, michango kutoka kwa marafiki na ndugu, kuuza rasilimali ulionayo, mikopo nafuu kutoka serikali hasa halmashauri.

KUHESHIMU/KUDHIBITI MUDA (TIME MANAGEMENT)

Hili ni jambo muhimu sana watu wengi hawatilii maanani suala la muda kudhibiti muda, siku zote ili uweze kufanikiwa lazima uheshimu muda, muda ni rasilimali ambayo haitoshi kila siku hivyo basi kwenye maendeleo na kufanikiwa lazima uzingatiwe vijana wengi hushindwa kuendana na muda ndio maana hushindwa kufanikiwa hasa baada ya kuanza kunyanyuka kimaendeleo.

UDHIBITI MZURI YA PESA (FINANCIAL MANAGEMENT).

Ili uweze kufanikiwa lazima pia uwe na udhibiti mzuri wa pesa, siku zote kupata pesa ngumu ila kupoteza pesa lahisi na kurudisha pesa uliopoteza ndio ngumu zaidi. Hivyo basi lazima matumizi mazuri ya pesa yawepo ili ufanikiwe, ili uweze kudhibiti pesa vizuri kujua kiasi gani unaingiza na kipi unatumia.

HESHIMU WATU.

Kwenye biashara yoyote watu ni lasilimali muhimu sana ikiwa kama wateja, nguvu kazi, mawazo na ushauri ama kwa namna nyingine. Kutokana na umuhimu wao lazima tuheshimu watu ndio tufanikiwe, kuheshimu watu ikiwemo matumizi ya lugha mzuri kwa watu, ukarimu kwa watu na makalibisho mazuri kwa wateja.

KUWA NA MTAZAMO WA MBELE ZAIDI (BE VISIONARY)

Ili ufanikiwe lazima uwe na jicho Pana kujua kesho kipi kinaweza kuwa fursa au nafasi mzuri ya kupata pesa. Mfanya biashara au mjasiriamali pia unatakiwa kuwa hivyo muda wote, ili kufanikiwa kiuchumi.

HITIMISHO
Watu wengi wamekuwa wakijishikisha katika Imani potofu juu ya kupata maendeleo mafanikio, baadhi ya wengi wametawaliwa na Imani potofu na kujua nguvu za Giza ndio kila kitu kuhusu mafanikio. Kumbe ni jambo linalowezekana kwa kirahisi zaidi. Kama kijana hupaswi kukata tamaa.

Prepared by
Maliki kilume
mallikkillume05@gmail.com
0685344373/0715014737.
 
Uzi mzuri ila nikiusoma between the lines upo centered kwenye maswala ya biashara..
Vipi kwa upande ambao ni wafanyakazi wa maofisini ambao hawako vizuri kwenye biashara
 
Uzi mzuri ila nikiusoma between the lines upo centered kwenye maswala ya biashara..
Vipi kwa upande ambao ni wafanyakazi wa maofisini ambao hawako vizuri kwenye biashara
Asante sana
 
Uzi mzuri ila nikiusoma between the lines upo centered kwenye maswala ya biashara..
Vipi kwa upande ambao ni wafanyakazi wa maofisini ambao hawako vizuri kwenye biashara
Wote TU, itawasaidia maana maelezo yameanza tangu namna ya kupata fursa Kisha mtaji na kuendelea
 
Uzi mzuri ila nikiusoma between the lines upo centered kwenye maswala ya biashara..
Vipi kwa upande ambao ni wafanyakazi wa maofisini ambao hawako vizuri kwenye biashara
Tena wafanya kazi ndio wanaweza kuitumia vizuri hii
 
Hii post inaweza kuwanufaisha watu wa aina yote kwa kijana usiogope kujalibu mwanzo Huwa mgumu
 
Wafanyakaz ishu n kuwa na matumiz mazur tu ya ela, kama hana uwezo wa kuzifanya zizae.
 
Wafanyakaz ishu n kuwa na matumiz mazur tu ya ela, kama hana uwezo wa kuzifanya zizae.
Wafanya kazi wengi sana wanajiamini kuwa wana chanzo Cha kudumu Cha pesa ambacho ni mshahara wao. Ukiangalia wafanya kazi wanayumba baada ya kustaafu
 
Ni kwel coz wengi wao wanakuyana na burungutu la pesa katika umri mbovu sana, so hata ile thinking capacity ya afanyeje, haipo tena. Wanaishia kutumia na kuishiwa tu.
Wenye bahati n wale wanaotumia na kufa chap[emoji16][emoji16]
Ila wale akina methusela wanaoishi miaka ya kucheba obvious hukutana na kipondo cha maisha
 
Mtoa post wew ni zaidi ya daudi aliempiga jiwe gorriati umetisha sanaa
 
Ni kwel coz wengi wao wanakuyana na burungutu la pesa katika umri mbovu sana, so hata ile thinking capacity ya afanyeje, haipo tena. Wanaishia kutumia na kuishiwa tu.
Wenye bahati n wale wanaotumia na kufa chap[emoji16][emoji16]
Ila wale akina methusela wanaoishi miaka ya kucheba obvious hukutana na kipondo cha maisha
Asante San mkuu wa mchango mzuri
 
Back
Top Bottom