realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Mara nyingi tunaona na tunasikia kwenye vyombo vya habari kuhusu Wosia kupingwa Mahakamani kutokana na utata wa wosia huo.
Hali hii husababisha kesi ya Mirathi kutumia muda mrefu hadi kukamilika kwake. Huku ukizingatia Mali ambazo walipaswa kugawana katika familia kukaa tu na pengine kuharibika.
Hata wenye haki ya kupewa mali hizo kushindwa kupewa kwa wakati. Lakini pia kesi inapokuwa Mahakamani watu hukosa utulivu wa akili (Msongo wa mawazo) pamoja na kuendelea kupoteza muda.
Soma Pia: Hatua na Taratibu za Kufungua Maombi ya kusimamia Mirathi Mahakamani
Je wananchi wana uelewa kuhusu uandishi wa wosia wenye vigezo au hujiandikia tu?
Vipi kwa wale ambao hawakuacha wosia?
Ili Mahakama iamini wosia huo unapaswa kuwa umezingatia nini?