Waheshimiwa nawashukuru kwa kuchangia hoja inayohusu uhuru wa habari.
Naona wazi kuwa kuna watu wanaofikiri CCM na Mafisadi wao wamelala. Kwa hakika hawa watu wako busy na wanatafuta kwa bidii kunyamazisha kila sauti inayowaamsha watanzania.
Lakini kwa kuwa nimepata taarifa nyingi kuwa Katibu Mgosi anapewaga habari zote zinazopita hapa JF nami kupitia hapa hapa ninampa ujumbe mfupi wa kudumu (UMK).
Mkubwa waweza kuendelea na kazi yako ya kuwashambulia watanzania wazalendo kwa kila lugha za kejeli na ubabe. waweza pia kuendelea kutumia fedha zao wanazokamuliwa, kudhalilisha haki zao na utu wao. Haya yote waweza kufanya kwa muda mfupi sana. Lakini kama jinsi ambavyo haiwezekani kuzuia jua kuchwa, saa inakuja na kila mtu atajua yaliyofanywa na wakubwa hawa. hapa ndipio mgosi atapewa heshima inayomstahili na Zitto, Slaa, Ndesamburo + Hamad Rashid watapokea yao.
Kwa UMK hiyo nakushauri kaka mgosi uanze kufikiria mbali na kutamane heshima ya wajukuu na vitukuu vyako.
Naapa!!!! Haki ya Mungu lazima kitakuja kizazi kitakachotaka kujua viongozi wa CCM wa sasa walikuwaje hadi kuwalinda na kuwatandikia mazulia mekundu mafisadi.
Kwaheri