LGE2024 Ilikuwa dhahhiri kuwa CCM 'ingeshinda'

LGE2024 Ilikuwa dhahhiri kuwa CCM 'ingeshinda'

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Kama kuna mtu alitegemea CCM kubwagwa kwenye uchaguzi unaoendelea, basi ana tatizo.

Hata kushiriki kwa wapinzani ni tatizo. Mshaambiwa uchaguzi unasimamiwa na TAMISEMI mwenye chama na machawa.

Sasa kwa mtaji huu upinzani ungeshinda nini na vipi? Dawa ya uchaguzi nchini ni kuiacha CCM na vyama machawa waendelee na mchezo wao hadi wadanganyika watakapoamka usingizini au kufufuka kama alivyowahi kusema Kamau wa Ngengi aka Jomo Kenyatta aliyezoea kusema kuwa mchonga alikuwa akitawala maiti wakati yeye akitawala manyang'au.

PIA SOMA
- LGE2024 - News Alert: - CCM yashinda 98.83% Wenyeviti Serikali za Mitaa
 
Kama kuna mtu alitegemea CCM kubwagwa kwenye uchafuzi unaoendelea, basi ana tatizo. Hata kushiriki kwa wapinzani ni tatizo. Mshaambiwa uchaguzi unasimamiwa na mkwe wa mwenye chama na machawa. Sasa kwa mtaji huu upinzani ungeshinda nini na vipi? Dawa ya uchafuzi nchini ni kuiacha CCM na vyama machawa waendelee na mchezo wao hadi wadanganyika watakapoamka usingizini au kufufuka kama alivyowahi kusema Kamau wa Ngengi aka Jomo Kenyatta aliyezoea kusema kuwa mchonga alikuwa akitawala maiti wakati yeye akitawala manyang'au.
uchaguzi Tanzania hata usimamiwe na mbowe, lipumba, zito kabwe na Hashim Rungwe Spunda,

CCM ushindi wa kishindo ni Lazima 🐒
 
Ndio maana mm binafsi sikuona umuhimu wa kwenda kupoteza muda wangu kupiga kura maana niliingia mitandaoni nikaona yanayojiri mikoa mbali mbali nikajua mshindi na mm niendelee na mishe zangu.
 
Huu si uchaguzi wa ccm kujisifu na kusifiwa kuwa imeshinda kwa kishindo kikubwa. Tunaangalia ushindani ulikuaje katika usawa wa kushindana kwa haki na uwazi. Uchaguzi umejaa abrakadabra nyingi halafu useme ccm imeshinda ushindi mkubwa? Kama ingeshinda walau kwa 60% na zilizobaki waachiwe wapinzani hapo tungeweza kukipongeza chama hicho kuwa kimepata ushindi mkubwa
 
Back
Top Bottom