Kama kuna mtu alitegemea CCM kubwagwa kwenye uchafuzi unaoendelea, basi ana tatizo. Hata kushiriki kwa wapinzani ni tatizo. Mshaambiwa uchaguzi unasimamiwa na mkwe wa mwenye chama na machawa. Sasa kwa mtaji huu upinzani ungeshinda nini na vipi? Dawa ya uchafuzi nchini ni kuiacha CCM na vyama machawa waendelee na mchezo wao hadi wadanganyika watakapoamka usingizini au kufufuka kama alivyowahi kusema Kamau wa Ngengi aka Jomo Kenyatta aliyezoea kusema kuwa mchonga alikuwa akitawala maiti wakati yeye akitawala manyang'au.