Ilikuwa mwaka 1981

Dah... Enzi hizo kupata dem lazima u andike barua.... Wengine wamezitunza hadi Leo.... Na wewe unazo?
Ilikuwa raha sana, ukiwa na girl friend ni simu za TTCL au unaenda kwao kuomba maji ya kunywa, akitoka dada unamuuliza Fulani yupo? Akitoka mama au baba unakunywa maji hata kama huna kiu unaondoka.
 
Vijana jazz usiwasahau. Pia unawakumbuka wakina Bichuka, Shabani Dede.
Sikinde sogea ukae, watu njatanjata , miaka Hiyo komando hamza anakwenda kung'oa mtoto wa Mzee cheyo tajiri, bendi Ni bendi kweli Hiyo kigogo lodge husogei akina kajamba nani acheni tu laizoni Viatu, suruali za bugaruu suspender kiunoni .
 
Bima Lee
Watunjatanjata 'washirika'
'Air pambamoto' Vijana

Mambo ya long
Sikuzile Bima Lee ilikuwa ikimilikiwa na Shirika La Bima La Taifa ( National Insurance Corporation, NIC), bendi hii ilitikisa vilivyo enzi zake, ilikuwa inakusanya nguli wengi wenye uwezo wa hali ya juu na waliochangia mafanikio makubwa katika bendi hiyo.
Miongoni mwa nguli hao, kulikuwa na waimbaji kama vile, Shaaban Dede ‘Super Motisha’, Othman Momba ‘Sauti ya Chuma’, Jerry Nashon ‘Dudumizi’ na Roy Bashekanako, na wenigine wengi.
Kwa upande wa ala, Bima lee ilikuwa imekusanya ‘mafundi’ kemkemu, kama akina Joseph Mulenga ’Spoiler’, Abdallah Gama, Suleiman Mwanyiro ‘Computer’, Hamis Mnyupe, Shaaban Lendi pamoja na Ally Rashid.
 
Hapo ilikua Bima Lee Ndio utasikia vibao kama Makulata nakutafuta sikuoni, kimurimuri, pesa zinasumbua acheni tu Raha ilikuapo zamani.
 
Ilikuwa raha sana, ukiwa na girl friend ni simu za TTCL au unaenda kwao kuomba maji ya kunywa, akitoka dada unamuuliza Fulani yupo? Akitoka mama au baba unakunywa maji hata kama huna kiu unaondoka.
Umenikumbusha mbali sana mkuu.
Hii ilwahi nitokea pale maeneo ya bamaga miaka ileeeee..... Nilisahau lazimika kununua maziwa (mtindi) pale nilipienda kuzoza, kisha nikamkuta Baba wa binti ndio yupo dukani.
Alafu bahati yangu mbaya, hiyo pesa (ilikua shilingi 10 ya noti) nilikua nimetumwa nikanunue chumvi dukani.....[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kulikuwa na kijana mmoja alikuwa anakuja nyumbani jioni, alikuwa anatrot akifika getini anaomba maji kwa mlinzi, mlinzi akija aniambia mgeni wako amefika, kama msure yupo inabidi mlinzi apewe maji.
 
Mkuu enzi hizo hapo Lang'ata social hall kulikua ma ma dj's Chriss phabby na Young millionaire.
 
Dah... Ulisalimika na kichapo siku hiyo?? [emoji13] [emoji13]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…