Ilikuwa sahihi Serengeti boys kuahidiwa zawadi ya kitita cha pesa

Ilikuwa sahihi Serengeti boys kuahidiwa zawadi ya kitita cha pesa

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,227
Reaction score
6,670
Nilijiuliza toka awali kama ilikuwa sahihi pale Mlezi wa Serengeti Boys, Mh Mengi alipotoa ahadi kwa wachezaji wa Setengeti Boys ya kitita cha TZS 20m/- kila mmoja kama timu ingefuzu kuingia fainali kombe la dunia na TZS 5m/- kwa mchezaji ambaye angefunga goli la kwanza katika mashindano yanayoendelea.

Nilijiuliza kama ilikuwa sahihi kwa kuzingatia kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa timu zaidi ya uwezo wa mchezaji mmoja mmoja. Hivyo basi, je, kila mchezaji aliichukulia ahadi hiyi kwa uzito upi; wa kitimu au wa kibinafsi!

Vivyo hivyo tumeshuhudia matokeo ya mchezo wa Timu ya Simba huko Kongo ambapo pia waliahidiwa zawadi ya fedha.

Pesa kamwe haijawa msingi wa maendeleo.

NAWASILISHA.
 
Inaleta maana sana kama fedha wanazoahidiwa zinakuwa kwa wachezaji wote na si mmoja mmoja.Hakuna mchezaji anaefunga mpira kwa juhudi zake ni lazima apewe pasi kutoka kwa wenzake.Mpira ni timu na zawadi lazima iwe ya timu yote.
 
Toa msaada wa aina yoyote kwa timu ili kuwahimiza umuhimu wa ushindi ila ahadi ni siri na ni baada ya matokeo .
 
Dr Mengi angetoa ahadi ya kutoa elimu kwa kila fani aipendayo mchezaji husika
 
Dr Mengi angetoa ahadi ya kutoa elimu kwa kila fani aipendayo mchezaji husika
 
walio ahidi mamilioni ndiyo hao hao walio hujumu tim.......
 
Back
Top Bottom